SHIRIKA LA AFYA DUNIANI (WHO) LASEMA TIBA YA CORONA BADO NI KITENDAWILI


Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema huenda kusiwepo tiba ya haraka ya Ugonjwa wa Covid-19 na kwamba itachukua muda mrefu kabla hali kurudi  kuwa ya kawaida katika baadhi ya  maeneo mbalimbali duniani.

Takwimu zinaonesha kuwa watu miliomi 18 kote duniani wameambukizwa virusi vinavyosababisha homa ya mapafu ‘Corona’ na karibu laki 7 wamefariki dunia.

Mkurugenzi wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus amezitaka nchi zote kutilia mkazo hatua za kiafya za kuzuia kusambaa kwa virusi hivyo.

Naye Mkuu wa Masuala ya Dharura katika Shirika hilo, Mike Ryan amesema nchi zenye kiwango kikubwa cha maambukizi zinastahili kujiandaa kwa mapambano makubwa.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527