RIDHIWAN KIKWETE AREJESHA FOMU YA KUGOMBEA UBUNGE CHALINZE, ASEMA: 'KAZI INAENDELEA'


Na Andrew Chale - Chalinze
KADA wa Chama Cha Mapinduzi CCM na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete leo 25 Agosti, amerejesha fomu ya kugombea Ubunge jimbo hilo kwa mara nyingine tena.

Ridhiwani amerejesha fomu hizo na kupokelewa kwa Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Chalinze, Ramadhan Posi.

Ridhiwani amesema wamejiandaa kufanya kampeni za staa ambazo zitakuwa za  kunadi sera na kuendeleza yale aliyoanzisha awali.

"CCM imejipanga kuendeleza kampeni za kistaarabu. Sisi hapa Chalinze Kazi inaendelea."Alisema Ridhiwani.

Miongoni mwa mambo atakayoendeleza ni pamoja na miundombinu, elimu, afya na maji.

Pia amesema kumalizia kiporo cha Kituo cha Afya Kibindu pamoja na 
Pia kumalizia Hospitali ya Wilaya ya Chalinze katika awamu zake nne zilizobaki.

"Tunataka suala la maji liwe la mfano kwani awali hapakuwa na huduma za maji Chalinze. kwa sasa tumepiga hatua maji yanapatikana katika karibu vijiji vingi. 

Lakini pia kuweka utaratibu wa maji yale yaweze kuleta vipato kwa Wananchi." Alisema Ridhiwani.

Aidha, amesema msemo wa "Kazi zinaendelea"  ni kwa sasa ni hatua ya kuubadilisha mji wa Chalinze na kuwa wa mfano  ikiwemo miundombinu ya kisasa pamoja na ujenzi wa stendi ya mabasi.

Wanachama wa CCM wakimsindikiza Ridhiwani Kikwete wakati wa kurejesha fomu hizo ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Chalinze.
Msimamizi wa Uchaguzi  Jimbo la Chalinze,  Ramadhan Posi akipokea risiti ya malipo ya taratibu za uchaguzi kwa Wabunge, kutoka kwa Mgombea Ubunge, Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete kwa tiketi ya CCM,  mapema leo 25 Agosti,2020.
Mgombea Ubunge wa jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM, Ridhiwani Kikwete akijadiliana jambo na viongozi wa CCM Wilaya ya Chalinze mara baada ya kurejesha fomu

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527