RAIS UHURU KENYATTA WA KENYA AWATAKA MAWAZIRI KUCHUKUA LIKIZO YA LAZIMA


Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amewataka mawaziri wote pamoja na makatibu katika wizara kuchukua likizo ya mapumziko ya lazima huku kukiwa na taarifa za mabadiliko kwenye baraza la mawaziri.

Rais Kenyatta amesema kuwa mawaziri na makatibu watalazimika kushughulikia majukumu ya dharura.

Kwa mujibu wa barua iliyotumwa na mkuu wa utumishi wa umma Joseph Kiyua likizo hiyo ya siku 11 itaanza Agosti 17 hadi agosti 28, mwaka huu ambapo mawaziri hawatafanya ziara za kukagua miradi na mipango ya serikali.

Likizo hiyo ya mawaziri na makatibu inakuja huku kukiwa kuna taarifa kuhusu Rais Kenyatta kuifanyia mabadiliko baraza la mawaziri.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527