NEC YATUPILIA MBALI MAPINGAMIZI YA TUNDU LISSU DHIDI YA DKT. MAGUFULI NA PROF. LIPUMBA | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, August 27, 2020

NEC YATUPILIA MBALI MAPINGAMIZI YA TUNDU LISSU DHIDI YA DKT. MAGUFULI NA PROF. LIPUMBA

  Malunde       Thursday, August 27, 2020

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetupilia mbali mapingamizi yaliyowekwa dhidi ya wagombea wa Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Magufuli na Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba.


Jana mgombea wa nafasi hiyo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu aliwasilisha mapingamizi hayo akidai kuwa wagombea hao hawakufuata kanuni na sheria za uchaguzi.

Lissu ameeleza kuwa Prof. Lipumba hakurudisha fomu za uteuzi kwa mujibu wa masharti yaliyowekwa na sheria. Pia, Lissu ameeleza kuwa Dkt. Magufuli hakuambatanisha picha kwenye fomu ya uteuzi na hakurudisha fomu kwa mujibu wa masharti yaliyowekwa na sheria.

Akitoa uamuzi wa NEC, Mkurugenzi wa Uchaguzi, Wilson Mahera amesema kuwa utetezi uliowasilishwa na wagombea hao umeidhihirishia tume kuwa mapingamizi hayo hayana msingi na yametupiliwa mbali.

Kufuatia uamuzi huo, Prof. Lipumba anaendelea kuwa mgombea halali kupitia CUF na Dkt. Magufuli anabaki kuwa mgombea halali kupitia CCM.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post