NEC YAMTEUA BERNARD MEMBE KUWA MGOMBEA URAIS WA TANZANIA KUPITIA ACT-WAZALENDO


Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imemteua Bernard Membe kuwa mgombea urais wa Tanzania kupitia ACT-Wazalendo na mgombea mwenza, Profesa Omar Fakih Hamad kwenye Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 28, 2020.

Membe na mgombea wake mwenza, Profesa Hamad wameteuliwa leo Jumanne tarehe 25 Agosti 2020 na Mwenyekiti wa NEC, Jaji Semistocles Kaijage katika ofisi za tume hiyo jijini Dodoma.

Membe aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya nje wa Tanzania kati ya mwaka 2007 hadi 2015 enzi za utawala wa Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete, amekuwa mgombea wa tisa kuteuliwa na tume hiyo.

Wagombea wengine waliokwisha rejesha fomu na kuteuliwa ni; Rais John Pombe Magufuli (CCM), Leopard Mahona (NRA), John Shibuda (Ada Tadea), Mutamwega Mgaiwa (SAU), Cecilia Augustino Mwanga (Demokrasia Makini), Yeremia Maganja (NCCR-Mageuzi), Ibrahim Lipumba (CUF) na Philip John Fumbo wa DP.

Vyama vilivyojitokeza kuchukua fomu vilikuwa 17 na mpaka sasa vimerejesha tisa bado nane. Mwisho wa urejeshaji kwa mujibu wa NEC ni saa 10 jioni.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527