NAIBU WAZIRI MHE.KANYASU AIAGIZA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII KUTOA KITALU CHA UWINDAJI WA KITALII KWA CHUO

 

Naibu Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii Mhe. Constantine J. Kanyasu akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Bodi ya Magavana wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori, MWEKA wakati wa Hafla ya Uzinduzi wa hafla hiyo  iliyofanyika Chuoni hapo Mkoani Kilimanjaro.
Naibu Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii Mhe. Constantine J. Kanyasu akimkabidhi begi lenye vitendea kazi Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt.Aloyce  Nzuki  mara baada ya Uzinduzi wa Bodi ya Magavana ya Chuo Cha Usimamizi wa Wanyamapori, Mweka  iliyofanyika  Mkoani Kilimanjaro.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Constantine J. Kanyasu akimkabidhi  begi yenye vitendea kazi Mwenyekiti wa Bodi ya Magavana wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori, Mweka, Prof. Faustine  Bee wakati wa Hafla ya Uzinduzi wa Bodi hiyo iliyofanyika jana katika Chuo hicho kilichopo Mkoani Kilimanjaro
Naibu Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii Mhe. Constantine J. Kanyasu akiwa katika picha ya pamoja na baadhi  ya Magavana wa Chuo Cha Usimamizi wa Wanyamapori, Mweka kilichopo mkoani Kilimanjaro  mara baada ya kuzindua Bodi ya Usimamizi wa Wanyamapori, Mweka, Wengi ni Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu ameamuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii kutoa  kitalu cha Uwindaji wa Kitalii kwa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori, Mweka  ili kitumike kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi wanaosomea masomo ya Uwindaji Bingwa        (Professional Hunters)

Ametoa agizo hilo leo wakati akizindua Bodi ya Magavana ya Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori, Mweka kilichopo katika wilaya  ya Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Mhe. Kanyasu amesema Kitalu hicho Uwindaji wa kitalii kitakisaidia Chuo hicho  kuzalisha wataalamu  wenye sifa.

Amesema kwa sasa Mabingwa wa Uwindaji wa Kitalii wanaofanya kazi hiyo hapa nchini  ni raia wa kigeni na baadhi ya  Wazawa waliopo  ni Wazee.

Amesema kitalu hicho kitachochea kupata  Wataalamu wa kutosha ili kuweza kukabiliana na  uhaba wa Wataalamu wa fani hiyo.

 Aidha, Mhe. Kanyasu amesema Chuo hicho kitasaidia  kukabiliana na Wafugaji  wanaoingiza vitalu vya uwindaji wa kitalii  kwa vile vitalu vingi  bado vipo wazi hali inayopelekea Wafugaji wengi  kuingiza mifugo hivyo

Pia, Amesema Kitalu hicho hakitasaidia Wahitimu pekee kufanya mafunzo kwa vitendo bali  itasaidia Wanyamapori kuwa salama kwa sababu Chuo hicho kitakuwa na jukumu la kupambana na tatizo la ujangili.

 
Aidha, Mhe. Kanyasu amempongeza Mwenyekiti wa Bodi hiyo,  Prof. Faustine Bee kwa kuchaguliwa kwa awamu ya pili ya kuwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo pamoja na Magavana wa Bodi kwa asilimia kubwa kuteuliwwa tena kuendelea kukitumia Chuo hicho.

Awali, Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Jaffari Kidegesho amesema kwa  sasa Wanafunzi wa Chuo hicho wamekosa maeneo ya kufanyia mafunzo kwa vitendo kwa ajili ya uwindaji wa kitalii.

 Amesema mwanzo Chuo hicho kilikuwa kikiyatumia  Mapori ya Akiba kwa ajili ya mafunzo hayo ila kwa sasa mapori hayo  yamepandishwa hadhi na kuwa Hifadhi za Taifa hivyo katika Hifadhi hizo hakuna shughuli za kibindamu zinazoruhusiwa kufanyika kwa mujibu wa sheria.


 Naye, Mkuu wa Chuo cha Wanyamapori, Mweka, Prof. Jaffari Kidegesho amesema kitalu hicho kitasaidia kufanya mafunzo kwa vitendo na hivyo kutasaidia kuwaandaa wahitimu wenye sifa kulingana na mahitaji ya soko

Naye, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki amekitaka Chuo hicho kuboresha mtaala wa mafunzo hayo ili kuzalisha Wataalamu wataoweza kujibu changamoto za soko.


Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Kilimanjaro, Alhaji Rajabu Kundya  amesema suala la uhifadhi na utalii limekuwa na mchango mkubwa sana kwa uchumi wa Taifa hali iliyopelekea Tanzania kuwa na Uchumi.

 Amesema shughuli hizo wanazichukulia kwa uzito mkubwa na wanakithamini sana  Chuo hicho kwa mchango mkubwa wa kuzalisha Wasomi wenye weledi.

Itakumbukwa kuwa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka ndo chuo pekee nchini kinachotoa mafunzo ya Uwindaji Bingwa wa Kitalii (PH)

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527