MPINA AWATAKA WAWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA MIFUGO KUTAFUTA MASOKO YA UHAKIKA NA KUITUMIA VIZURI BANK YA MAENDELEO YA KILIMO

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina akiangalia moja ya dawa za mifugo katika kiwanda cha Farm Accesses Ltd cha mjini Arusha kinachotengeneza pembejeo za mifugo. Waziri Mpina alitembelea kiwanda hicho jana akiwa katika ziara ya kikazi
Waziri Luhaga Mpina, akiwa katika ziara ya kikazi  Mkoani Arusha na Kilimanjaro aliambatana na wajumbe na Mkurugenzi Mtendaji wa Bank ya Maendeleo ya Kilimo Bw. Japhet Justine (kushoto)

Waziri Luhaga Mpina katika ziara yake ya kikazi Mkoani Kilimanjaro na Arusha

Msajili wa bodi ya nyama kutoka katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw.Imani Sichwale alikipongeza kiwanda cha Meat King kwa kuzalisha nyama zilizo katika kiwango cha hali ya juu.

Na Mwandishi wetu, Arusha.


Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina amewataka wawekezaji katika sekta ya  Mifugo husasani wamiliki wa viwanda vya nyama nchini kutafuta masoko ya uhakika  ndani na nje ya nchi.


Waziri Mpina aliyasema hayo jijini Arusha alipokuwa katika ziara yake ya kikazi ya  kutembelea viwanda vya mazao ya mifugo ambapo alisema Serikali inawaunga mkono  wawekezaji katika sekta ya nyama na kushauri wafanye upanuzi wa viwanda vyao  kwani baada ya janga la covid 19 biashara sasa imeanza kurudi vizuri.

“Changamkieni masoko na ziwepo products zote  katika masoko ya ndani watanzani na  wageni wanahitaji wazipate.”Alisisitiza.

Akiwa katika kiwanda cha kuchakata nyama cha Meat king mjini Arusha Mpina aliwataka wafanye bidii katika kuhakikisha wanapata watu wanaoweza kuyafikia  masoko kwa kwenda au kuwatumia mawakala hasa katika mikoa ya Mwanza, Tanga na sehemu nyingine za nchi.

Katika ziara yake kiwandani hapo Waziri Mpina, aliishauri Bank ya Maendeleo ya Kilimo TADB kuangalia uwezekano wakupanua wigo wa mikopo ili viwanda viendelee  kuwepo sambamba na kuinua soko la ndani na kuimarisha mnyonyoro wa thamani  wanyama na kufanya bidhaa hizo ziwe na ushindani kimataifa, kutoa ajira kwa watanzania na wafugaji wazidi kuinuliwa kiuchumi.

Akiongea katika ziara hiyo ya Waziri Mpina, Kaimu Mkurugenzi wa mikopo na biashara  kutoka Bank ya Maendeleo ya Kilimo Bw. Jeremiah Muhanda, alisema Bank hiyo imeweza kuwasaidia wawekezaji kupata ,machine za kisasa, mitaji yakufanyia kazi na kuwasaidia mitaji wafugaji kupitia vikundi.

Na aliongeza kwa kusema kuwa Bank hiyo pia imewezesha kiwanda cha pembejeo za mifugo cha farm access cha mjini Arusha mkopo wa kiasi cha shilingi milioni mia nne tisini na tisa (499Milioni).

Kwa upande wake Msajili wa Bodi ya nyama nchini Bw. Imani Sichalwe alikipongeza  kiwanda cha kuchakata nyama cha Meat King kwa kuzalisha nyama yenye viwango vya juu ambapo awali ilikuwakiagizwa kutoka nje ya nchi.

Alipokuwa katika kiwanda cha maziwa cha Kilimanjaro Fresh Waziri  Mpina  alimpongeza muwekezaji huyo kwa kununua maziwa kwa wafugaji kwa bei nzuri ya  shilingi mia nane themanini (880/-) kwa lita ikiwemo kuwapongeza kwa kufanya kazi nzuri ya kuzalisha lita elfu nane (8000) mpaka elfu tisa(9000)kwa siku na maziwa hayo kufika katika kila maeneo nchini.

“Serikali itaendelea kuunga mkono na kusaidia kutatua changamoto zozote na msipate  vikwazo kwenye soko zuri la wafugaji wetu, ilikuweza kupata maziwa  mazuri na bora...Nawasihi pia mpanue masoko kadiri mnavyoweza, nawahakikishia masoko yaliyopo yataendelea kulindwa.” Alisema.

Aidha,Waziri Mpina alielekeza bodi ya maziwa kufuatilia maziwa yanayoingizwa toka nje ya nchi kinyume na utaratibu yaondolewe na walipe kodi za serikali na nchi isiwe dampo la kuingiza bidhaa hizo kinyume nataratibu.

Alipotembelea kiwanda cha nyama cha Elia Foods Overseas ltd kilichopo Wilayani  Longido,Waziri Mpina  alimpongeza muwekezaji huyo kwa kufanya uamuzi wa kujenga kiwanda hicho nchini.
 

Hata hivyo muwekezaji huyo alimuomba Waziri Mpina kushugulikia changamoto ya  kodi anayokabiliana nayo ili kuweza kuingiza vipuri toka nchi jirani ya Kenya na  kuanza uzalishaji kwawakati, ambapo katika hilo Waziri Mpina alielekeza dawati la  sekta binafsi la wizara yake kushughulikia changamoto hiyo mara moja ili uzalishaji katika kiwanda hicho uanze.

Ziara ya Waziri Mpina Mkoani Arusha ilihusisha kiwanda cha kuchakata nyama cha  Meat King, Elia Foods Overseas ltdnakiwanda cha maziwa cha Kilimanjaro Fresh.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post