Majukwa
yakiendelea kupambwa kwenye Uwanja wa Jamhuri Dodoma tayari kesho
Agosti 29,2020 kwa mkutano wa uzinduzi wa kampeni za Mgombea Urais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli pamoja na
Mgombea Mwenza, Samia Suluhu Hassan. Uchaguzi Mkuu utafanyika Oktoba
28 mwaka huu. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA.
Picha
za Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli zikiwa
zimepambwa kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma ambapo uzinduzi wa
kampeni za Uchaguzi Mkuu utafanyika kesho Jumamosi.
Kijana
muuza korosho Jamali Mohamed, akiangalia picha ya Mgombea Urais wa
Tganzania kupitia CCM, Dk. Magufuli iliyopambwa kwenye Uwanja wa
Jamhuri.
Mambo yalivyo Uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Bendera za Chama Cha Mapinduzi zikiwa zimelipamba Jiji la Dodoma.
Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527