RAIS MUSEVENI ATANGAZA SIKU YA KITAIFA YA MAOMBI KUHUSU CORONA...KAPEWA UJUMBE WA MAONO KUTOKA KWA MUNGU


Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametangaza siku ya kitaifa ya maombi kwa ajili ya Covid-19 itakayofanyika jumamosi Agosti 29, 2020.


Amesema wazo la kufanya hivyo amelipata kutoka kwa raia wa Uganda ambaye alikuwa na 'Maono kutoka kwa Mungu'.

"Kuna Mtu amenifuata na kuniambia Mungu kamuambia kwenye maono kwamba ninapaswa kuandaa maombi ya kitaifa ili Mungu atuepushe na corona, kwahiyo natangaza kuwa Aug 29,2020 ni siku ya maombi ya Kitaifa na pia itakuwa siku ya mapumziko, baki nyumbani kwako na uombe”" Museveni amesema katika ujumbe wake wa mtandao wa kijamii.

Hadi sasa Uganda imerekodi watu 2,679 wenye maambukizi ya virusi vya coronana na  vifo 28.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527