HALMASHAURI KUU YA CCM MKOA WA TANGA YAWAPITISHA WAGOMBEA 245 NGAZI YA UDIWANI


HALMASHAURI kuu CCM mkoa wa Tanga imewapitisha kwa kauli moja wagombea wote 245 walioomba kuwania nafasi ya udiwani katika wilaya zote nane mkoani hapo.



Hayo yalibainishwa na Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga Shaibu Akwilombe wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema kuwa katika kikao hicho cha Halmashauri kuu mkoa kilichofanyika Agosti 18 mwaka huu.

Alisema kikao hicho kiliamua kuwapitisha wagombea wote wa udiwani walioshika nafasi ya kwanza waliopitishwa katika kura za maoni na kwenye vikao husika vya kata wilaya kwa sababu kiliafikiana na maoni ya vikao hivyo.

Aidha alisema mkoa wa Tanga  una kata 245 zinazopatikana katika Halmshauri 11 ambapo kila kata ilitoa mgombea aliyeshinda kwa nafasi ya kwanza na kwamba katika mchakato huo hakuna aliyeshika nafasi ya pili na kupata fursa ya kuipeperusha bendera bali ni wale ambao walishinda kwenye kura za maoni ambao waliyepitishwa katika kikao hicho.

Alisema uamuzi huo umeweka rekodi ya kihistoria kwa wagombea wote waliopata nafasi ya kwanza kupitishwa katika kuwania nafasi hiyo ya udiwani na wapo waliopata nafasi ya pili na ya tatu na kuendelea lakini hawakuweza kukidhi  vigezo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527