KABURU ATAKA WANA CCM SINGIDA KUVUNJA MAKUNDI KUIPA USHINDI CCM | MALUNDE 1 BLOG

Friday, August 28, 2020

KABURU ATAKA WANA CCM SINGIDA KUVUNJA MAKUNDI KUIPA USHINDI CCM

  Malunde       Friday, August 28, 2020
Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida Ahmed Kaburu

Na Ismaily Luhamba, Singida.
KATIBU Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida Ahmed Kaburu amewaomba wagombea na wafuasi wa Chama hicho kuvunja makundi na kuungana kwa pamoja ili kukiwezesha chama kupata ushindi.

Kaburu ametoa rai hiyo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika kuelekea kwenye kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Aliwaomba wagombea wote wa majimbo nane kwa nafasi ya ubunge katika mkoa wa Singida pamoja na udiwani kuvunja makundi na kuungana kwa pamoja kwa lengo la kukiwezesha cha kupata ushindi kwa nafasi zote. My

"Niwaombe wagombea wote wa CCM Mkoa wetu wa Singida tushiriki kwenye kampeni,tuvunje makundi, Chama kwanza mtu baadaye", alisema Kaburu.

Alisema baada ya michakato yote hatimaye wamepatikana wagombea,hao ndiyo ambao Chama kimewapendekeza ili kupeperusha bendera ya CCM, hivyo wangine waliokosa nafasi hizo hawanabudi kuungana na wenzao na chama kwa ujumla kwani hatuwezi tukawa Viongozi wote tena kwa wakati mmoja.

Aidha Kaburu alisema Chama hicho kinaungana na tume ya uchaguzi katika kuhakikisha wanafanya kampeni za kiistaarabu kwani baada ya uchaguzi kuna maisha, hivyo chama kitazingatia maelekezo yote ya tume ya uchaguzi wakati wa kampeni na Uchaguzi.

Alisema Chama hicho Mkoa wa Singida kinatarajia kufungua rasmi kampeni zake Septemba tano mwaka huu katika uwanja wa Liti stadium awali ulikuwa unaitwa uwanja wa Namfua.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post