ALIYEKUWA RAIS WA MALI IBRAHIM BOUBACAR KEITA AACHILIWA HURU NA WANAJESHI WALIOASI | MALUNDE 1 BLOG

Friday, August 28, 2020

ALIYEKUWA RAIS WA MALI IBRAHIM BOUBACAR KEITA AACHILIWA HURU NA WANAJESHI WALIOASI

  Malunde       Friday, August 28, 2020

Aliye kuwa rais wa Mali, Ibrahim Boubacar Keita, aliyekamatwa Agosti 18 na kundi la wanajeshi lililofanya mapinduzi, ameachiliwa huru jana Alhamisi, jeshi limetangaza. 


Duru za kuaminika zinabaini kwamba mwanae, Karim Keita, alifaulu kuondoka nchini na kwa sasa yuko ukimbizini nje ya nchi.

Baraza kuu la kitaifa, lililoowekwa na wanajeshi kuiongoza nchi, "linaarifu wananchi wa Mali na jumuiya ya kimataifa kwamba aliye kuwa rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keïta ameachiliwa huru na kwa sasa yuko nyumbani kwake", CNSP imetangaza kwenye mtandao wa Facebook.

Aliye kuwa rais wa Mali yuko huru na anaweza kufanya shughuli zake na kutembea anapotaka. Kwa sasayuko nyumbani kwake kwa mujibu wa afisa mmoja wa kundi hilo la wanajeshi.

Mmoja kati ya ndugu zake, ambaye hakutaka jina lake litajwe, amesema IBK alirejea nyumbani kwake katika eneo la Sebenikoro wakati wa usiku.

Credit:RFI


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post