JAMII YATAKIWA KUFUATILIA TAARIFA ZA WANYAMA PORI NA WANYAMA WA NYUMBANI…MANJERENGA ASEMA ‘HAKUNA FISI ANAYEFUGWA NYUMBANI’


 Kushoto ni Afisa Maliasili na Mazingira Manispaa ya Shinyanga Bw. Ezra Manjerenga,Kamanda Mkuu Mstaafu wa Sungusungu Manispaa ya Shinyanga Bw. John Shimba Kadama,Afisa Mtafiti kutoka Taasisi ya Afya Ifakara na Afisa Mifugo Manispaa ya Shinyanga Bw. Chrispacy Kasimbazi wakiwa kwenye studio za Radio Faraja fm stereo 91.3 Shinyanga katika kipindi cha Mambo leo Kinachoongozwa na Mtangazaji Josephine Charles.Picha zote na Edward Mangu
Kushoto ni Afisa Maliasili na Mazingira Manispaa ya Shinyanga Bw. Ezra Manjerenga,Kamanda Mkuu Mstaafu wa Sungusungu Manispaa ya Shinyanga Bw. John Shimba Kadama,Afisa Mtafiti kutoka Taasisi ya Afya Ifakara na Afisa Mifugo Manispaa ya Shinyanga Bw. Chrispacy Kasimbazi wakiwa kwenye studio za Radio Faraja fm stereo 91.3 Shinyanga. 
Afisa Maliasili na Mazingira Manispaa ya Shinyanga Bw. Ezra Manjerenga akiwa kwenye mahojiano maalum katika kipindi cha Mambo Leo kinachorushwa na Radio Faraja fm stereo 91.3 Shinyanga.
 Afisa Mifugo Manispaa ya Shinyanga Bw. Chrispacy Kasimbazi akiwa kwenye mahojiano maalum katika kipindi cha Mambo Leo kinachorushwa na Radio Faraja fm stereo 91.3 Shinyanga.
Afisa Mtafiti kutoka Taasisi ya Afya Ifakara Joel Changalucha akiwa kwenye mahojiano maalum katika kipindi cha Mambo Leo kinachorushwa na Radio Faraja fm stereo 91.3 Shinyanga.
Kamanda Mkuu Mstaafu wa Sungusungu Manispaa ya Shinyanga Bw. John Shimba Kadama akiwa kwenye mahojiano maalum katika kipindi cha Mambo Leo kinachorushwa na Radio Faraja fm stereo 91.3 Shinyanga. 
Kutoka Kushoto ni Afisa Maliasili na Mazingira Manispaa ya Shinyanga Bw. Ezra Manjerenga,Kamanda Mkuu Mstaafu wa Sungusungu Manispaa ya Shinyanga Bw. John Shimba Kadama,Mtangazaji wa Kipindi cha Mambo leo Radio Faraja fm stereo Josephine Charles,Afisa Mifugo Manispaa ya Shinyanga Bw. Chrispacy Kasimbazi na Afisa Mtafiti kutoka Taasisi ya Afya Ifakara wakiwa katika picha ya Pamoja nje ya Studio za Radio Faraja baada ya Kipindi.

Picha zote na Edward Mangu



Na Mwandishi wetu - Malunde1 blog
Wito umetolewa kwa Jamii kufuatilia vyombo vya Habari ili kupata Elimu inayotolewa na wataalamu kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu Wanyama pori na wanyama wa nyumbani kama vile mbwa na paka.

Wito huo umetolewa leo na Maafisa wa Idara za Maliasili na Mazingira,Idara ya Mifugo,Pamoja na Afisa kutoka Idara ya Utafiti na Afya,ambao kila mmoja ametoa elimu kupitia kipindi cha Mambo Leo kinachorushwa na Redio Faraja fm Stereo kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa chini ya Mtangazaji Josephine Charles, juu ya mahusiano yaliyopo kati ya Wanyama pori,wanyama wa nyumbani na Binadamu pamoja na kutoa Elimu kuhusu ugonjwa wa Kichaa cha mbwa.

Akizungumza kupitia kipindi hicho Afisa Maliasili na Mazingira wa Manispaa ya Shinyanga bwana Ezra Manjerenga ametoa wito kwa Jamii kuondokana na dhana  potofu kwamba kuna fisi wanaofugwa majumbani na badala yake wanapobaini kuwepo kwa mnyama huyo watoe taarifa kwa mamlaka husika.

Kwa upande wake Afisa mifugo wa Manispaa ya Shinyanga Bwana  Chrispacy Kasimbazi ametumia nafasi hiyo kuwa hamasisha wakazi wa Mji wa Shinyanga kupeleka mifugo yao kupata chanjo ili kuwa kinga na kifafa cha mbwa,chanjo ambayo itaanza kutolewa kuanzia September Mosi hadi September 28 mwaka huu katika Manispaa ya Shinyanga.



Naye afisa mtafiti kutoka taasisi ya Afya Ifakara Bwana Joel Changalucha ameiomba jamii kutoa taarifa kwa Mamlaka au taasisi husika kupitia namba 0800750052 ambayo ukipiga ni bure ikiwemo idara ya mifugo pale Mbwa ama Paka wao wanapoonekana kuwa na dalili za kichaa cha mbwa ili hatua stahiki ziweze chukuliwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527