MAAMUZI YA ANDREW CHENGE BAADA YA KUPIGWA CHINI UBUNGE CCM

Andrew Chenge
Mbunge wa Jimbo la Bariadi mkoani Simiyu aliyemaliza muda wake Andrew Chenge, amesema kuwa kuanzia sasa ameyavunja makundi yote yaliyokuwa yakimuunga mkono yeye, badala yake watakuwa ni wamoja ili kumuunga mkono mgombea wa Jimbo hilo aliyepitishwa na CCM Mhandisi Andrea Kundo.

Chenge amewashukuru viongozi wote wa CCM waliompa nafasi ya kuongoza kwa kipindi cha miaka 15 ambayo aliitumia kukomboa jimbo hilo lisiende kwa wapinzani na kwamba ameamua kutoruhusu uwepo wa makundi hayo ili kuepuka anguko la kidemokrasia.

"Niwashukuru sana viongozi wa CCM kwa heshima mliyonipatia tangu 2005, naona kwenye mitandao maneno mengine ya kipuuzi yanasemwa pembeni, nasema kuanzia sasa hakuna kundi la Chenge, kundi letu ni la CCM", amesema Chenge.

Mwanasiasa huyo Andrew Chenge, amewahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi Serikalini ikiwemo Uwaziri na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post