ACT WAZALENDO YASISITIZA KAZI NA BATA...VYAMA VYA SIASA VYAKUMBUSHWA KUFUATA SHERIA

Kiongozi wa Chama Cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe 


Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kiongozi wa Chama Cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amesema vyama vya upinzani nchini Tanzania vimejipanga kikamilifu kuhakikisha vinapata ushindi mkubwa katika uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28,2020.

Zitto Kabwe ameyasema hayo leo kwenye Mkutano Mkuu  wa ACT Wazalendo Taifa unaofanyika jijini Dar es salaam.

"Sisi kama vyama vya upinzani tutaweka wagombea makini kuanzia ngazi ya Rais,Madiwani na Wabunge. Tutahakikisha tunashinda kwenye uchaguzi Mkuu 2020",amesema.

"Tutaendelea kufanya juhudi hadi za dakika za mwisho kuweka ushirikiano ili kupata ushindi katika uchaguzi.Vyama vya UpinzaniaTutakuwa wamoja,Inawezakana kufanya kazi huku tukila bata. Tunaamini katika Kazi na Bata",amesema Zitto Kabwe.

Naye Mwakilishi wa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Sisty Nyahoza amevitaka vyama vya siasa nchini kufuata sheria katika uchaguzi mkuu 2020.

"Mhe. Mwenyekiti fanyeni mbwembwe zote,propaganda zote kwa mujibu wa sheria. Hamuwezi kila chama mkafikia malengo yenu bila kufuata sheria. Tunawaasa uchaguzi uende kwa mujibu wa sheria",amesema Sisty.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post