TBS YAENDELEA KUTOA ELIMU KATIKA MAONESHO YA NANE NANE MKOANI SIMIYU


Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeendelea kutoa elimu kwa wananchi na wafanyabiashara katika Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea Nyakabindi Mkoani Simiyu ili kuweza kuwajengea uelewa namna TBS inavyoweza kutekeleza majukumu yake.


Akizungumza katika Maonesho hayo Mkurugenzi wa TBS, Dkt.Athuman Ngenya amesema wanaendelea kutoa elimu kwa wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla kuhusu usalama wa bidhaa na Chakula pamoja na kufanya usajili.

"Hapa hapa Nyakabindi tunafanya usajili wa online kwa hiyo wananchi wanaoishi maeneo haya wenye biashara ya Chakula na Vipodozi wanaweza wakaja hapa tukawaanzishia mchakato wa usajili na ikiwezekana tunaweza kwenda katika maeneo yao kwaajili ya kufanya ukaguzi". Amesema Dkt.Ngenya.

Aidha Dkt.Ngenya amewataka wenye maghala ya kuhifadhia chakula na wenye usafiri wa kusafirisha vyakula waweze kufika katika shirika hilo kwaajili ya kujisajili na kufanyiwa ukaguzi ili kuweza kufanya biashara ama kuhifadhi vyakula kwenye usalama.

"Wenye maghala ya kuhifadhi chakula au vyombo vya usafiri zinazobeba vyakula lazima waje kwetu TBS wajisajili ili waweze kufanya biashara hiyo katika hali nzuri". Amesema Dkt.Ngenya.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527