MGOMBEA URAIS ACT WAZALENDO KUJULIKANA AGOSTI 5 | MALUNDE 1 BLOG

Sunday, August 2, 2020

MGOMBEA URAIS ACT WAZALENDO KUJULIKANA AGOSTI 5

  Malunde       Sunday, August 2, 2020

Na Mwandishi Wetu

Chama cha ACT -Wazalendo kimepanga kutangaza wagombea wake wa Urais watakaopeperusha bendera zake Tanzania bara na Zanzibar, Agosti 5 mwaka huu.


Akitangaza vikao vya maandalizi kuelekea kufanyika kwa mkutano mkuu wa chama hicho, Dar es Salaam, Naibu Katibu wa mawasiliano na Uenezi wa ACT-Wazalendo, Janeth Lithe, alisema kuwa kikao cha maandalizi ya mkutano huo mkuu kilianza kwa Kamati Kuu iliyoketi mapema leo.

Alisema pamoja na masuala mengine, mkutano mkuu wa mwaka huu utakuwa na kazi kuu mbili amabazo ni pamoja na kuwapitisha rasmi wagombea Urais wawili, Zanzibar na Tanzania bara.

"Shughuli nyingine kubwa ya mkutano huo mkuu ni kuipitisha na kuizindua rasmi Ilani mpya  ya Uchaguzi ya ACT-Wazalendo ambayo imebeba matarajio mengi ya wananchi." alisema Lithe.

Aidha, Lithe aliongeza kuwa, suala la ushirikiano wa vyama vya upinzani linaendelea katika ngazi ya majadiliano, na likifikia mahali pa kuwatangazia Watanzania watajulishwa rasmi.

"Suala la ushirikiano ni muhimu kwakuwa nila maslahi zaidi ya chama kimoja kusimama peke yake.

"Na hili si kwa ajili ya kuungana na Chadema tu, bali na vyama vingine vyenye malengo ya kuiondoa CCM madarakani" alisisitiza.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post