WANAMICHEZO CHUO CHA SAYANSI ZA AFYA KOLANDOTO WAADHIMISHA SIKUKUU YA NANE NANE KWA MECHI YA KIRAFIKI

Wachezaji wa Timu zote mbili zilizoshiriki kucheza mechi ya Kirafiki ya Mpira wa Miguu kati ya Wachezaji wq Mpira wa Kikapu(Basketball) na wachezaji wa mpira wa Miguu(Football) wakiwa katika picha ya Pamoja kabla ya mtanange huo kuanza katika uwanja wa Mpira wa Miguu wa Shule ya Msingi Kolandoto Mkoani Shinyanga.

Na Josephine Charles - Malunde1 blog
Katika kuadhimisha sikukuu ya Wakulima (Nanenane) mwaka 2020,wachezaji wa Mpira wa Miguu(football) na wachezaji wa mpira wa Kikapu (Basketball) kutoka Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto na baadhi ya Wafanyakazi wa Hospitali ya Kolandoto mkoani Shinyanga,wamecheza mechi ya kirafiki ya mpira wa Miguu katika uwanja wa Shule ya Msingi Kolandoto.

Mechi hiyo ilianza kuchezwa majira ya saa kumi na moja jioni na kumalizika saa moja usiku, baada ya Dakika 90 kuisha timu zote mbili zilitoka sare ya bao moja kwa moja.


Awali kipindi cha kwanza cha mchezo huo kiliisha kwa sare ya bila bila,ambapo katika kipindi cha pili dakika ya 50 wacheza mpira wa miguu(footballers) walipata goli la kwanza lililofungwa na Ibrahimu Makongoro na katika dakika ya 86 ya mchezo huo wacheza mpira wa kikapu(Basketballers)wakalipa deni kwa kufunga goli moja ambalo lilifungwa na John Magere.

Baada ya dakika 90 kuisha wakaelekea katika mikwaju ya Penalti ili kumpata mshindi wa mechi hiyo,hivyo wacheza mpira wa Kikapu(Basketballers) wakaibuka na ushindi kwa kupata penalt 4 dhidi ya wacheza mpira wa miguu(footballers) kupata penalt mbili.
Baadhi ya Wachezaji wa Mpira wa Kikapu walioshiriki mchezo wa Kirafiki wa Mpira wa Miguu wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo kuanza.
Baadhi ya Wachezaji wa Mpira wa Miguu wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo kuanza.
Wachezaji wa Timu zote mbili zilizoshiriki kucheza mechi ya Kirafiki ya Mpira wa Miguu kati ya Wacheza Mpira wa Kikapu(Basketball) na wachezaji wa mpira wa Miguu(Football) wakiwa katika picha ya Pamoja kabla ya mtanange huo kuanza katika uwanja wa Mpira wa Miguu wa Shule ya Msingi Kolandoto mkoani Shinyanga.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527