VETA yaja na teknolojia mpya kutibu maumivu ya mgongo. | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, August 8, 2020

VETA yaja na teknolojia mpya kutibu maumivu ya mgongo.

  Malunde       Saturday, August 8, 2020
Na Samirah Yusuph
Chuo Cha ufundi stadi VETA kimekuja na mbinu mpya kwa kutengeneza kitanda maalumu kea ajili ya kutibu maumivu ya mgogo.

Kitanda hicho kimetengenezwa kwa ajili ya kuwasaidia watu wenye maumivu ya mgogo ambacho hakitumii nishatati ya umeme na kimetengenezwa na mafundi seremala.

Oswin Komba mkurugenzi wa kituo cha kulea wahitimu wa uselemala OSARIKO WOOD WORK LTD /VETA kilichopo Temeke dar es salaam akiwa katika maonyesho ya nane nane Nyakabindi mkoani Simiyu amesema kitanda hicho Ni Bora kwa kuondoa maumivu.

"kitanda hiki Ni tiba kwa watu wenye matatizo ya  kiuno, mbavu na mgongo  na wakikitumia wanapona kabisa badala ya kulala sakafuni,"

 Alisema kitanda hicho kinasaidia kubadilisha hali ya hewa na kuleta hewa safi ikiwa kitawekwa kwenye chumba kidogo chenye uwezo mdogo wa kubadilisha hewa.

 Chini ya kitanda hicho Kuna  mkaa wa mianzi ambao husaidia kufyonza sumu iliyoko kwenye hewa pia kuna ceiling board na godoro jembamba ambavyo

 Alisema kwa matumizi ya mkaa iliyo katika kitanda hicho inaweza kuchukua miezi mitatu Hadi sita kubadirisha kutokana na ukubwa wa chumba.

 Aidha aliongeza kuwa mabaki ya mkaa ulioisha matumizi katika kitanda tiba yanaweza kutumika katika matumizi mengine ya nyumbani.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post