HAWA NDIYO WASHINDI UCHAGUZI KURA ZA MAONI MADIWANI VITI MAALUM SHINYANGA MJINI Mshindi wa Kura za  maoni  tarafa ya mjini Shella Mshandete(Kushoto) na  Zuhura Waziri (Kulia) Mshindi wa kura za Maoni Udiwani viti maalum Tarafa ya Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga wakifurahia baada ya ushindi wao.


Na Shinyanga Press Club Blog 
Mchakato wa Kuwapata Madiwani wa viti Maalum ndani ya Chama cha Mapinduzi CCM umefanyika leo nchini ambapo mkoani  Shinyanga pia zoezi hilo limefanyika  na  Jimbo la  Shinyanga mjini limekamilisha zoezi hilo kwa kuwapigia kura za maoni Wagombea  29  waliojitokeza  kuwania nafasi hiyo

Akitangaza  Matokeo  ya kura hizo Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Shinyanga Mjini ambaye ni Mkuu wa Wilaya hiyo,  Mh. Jasinta Mboneko amesema kuwa kura hizo si ushindi bali  ni mchakato wa mwanzo kuelekea kuwapata watakaopeperusha bendera ya chama hicho.
Ambapo Tarafa ya Mjini iliyokuwa na Wagombea 20 washindi waliopatikana  ni  Kanji Moshi  aliyepata kura 152, Seni Paschazia  amepata kura 112, Ester Makune  amepata kura 108 na  Shella Mshandete amepata  kura  103.  

Huku  Pika Shongole  kutoka Tarafa ya Old Shinyanga akiibuka na ushindi wa Kura 111 dhidi ya wapinzani wake wawili na Zuhura Waziri akiibuka Mshindi toka Tarafa ya Ibadakuli aliyepata kura 162 dhidi ya wapinzani wake wawili.

Mboneko amesema kuwa jumla ya Wajumbe 192 wamepiga kura kati ya 198 waliopaswa kuhudhuria  na kubainisha kuwa  jumla ya tarafa tatu   zimeshiriki katika uchaguzi huo ambazo ni  Old Shinyanga  ambapo wamejitokeza wagombea watatu ambao ni Nyasamba Mussa  aliyepata kura tatu, Swedi Abdul kura 84 na Chongole  Pika kura  111.

Aidha  katika  tarafa ya  Ibadakuli   waliogombea ni watu watatu ambao ni Kawani Mdaki aliyepata kura 12, Regina  Enock kura 34 na Zuhura Waziri kura 162.

Kwa upande wa Tarafa ya mjini  wagombea 20 wa tarafa ya mjini wamejitokeza kati yao washindi wanne wa kura za Juu ndiyo wamepitishwa kuwa washindi akiwemo   Seni Paschazia aliyepata  kura 112,  Ester Makune kura  108, Shella Mshandete kura 103 na   Kanji Moshi kura  152.

Mwenyekiti  wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT)  Wilaya ya Shinyanga Mjini,   Shumbuo Katambi amewataka  wajumbe kuacha makundi  yaliyokuwepo badala yake washikamane    ili kuleta ushindi wa chama cha mapinduzi kuelekea uchaguzi mkuu.

Shambuo ameongeza kuwa kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu wanawake ni jeshi kubwa hivyo wanapaswa kuhakikisha wanasimama imara katika kuleta ushindi wa CCM unaotarajiwa kufanyika  Octoba 28  Mwaka huu

Naye mmoja wa Wagombea aliyeshinda kura hizo za maoni Bi Zuhura Waziri amesema kuwa kurejea kwake kwa mara ya pili baada ya kupitishwa na wajumbe wa chama hicho ni ishara ya utendaji kazi bora kwa wanachama na wananchi wa tarafa ya Ibadakuli hivyo ataitumia fursa hiyo kwa mara nyingine kwenda kusukuma gurudumu la maendeleo katika tarafa yake.

 Baadhi ya Wagombea wa Udiwani Viti Maalum Manispaa ya Shinyanga wakiwa wameketi wakiendelea kusubiri mchakato wa Upigaji Kura za  Maoni.
 Wajumbe wakisubiri kutekeleza wajibu wao wa kuwapigia kura wagombea 
Katikati ni Mgombea wa Nafasi ya udiwani Viti maalum toka Tarafa  ya Ibadakuli Zuhura Waziri akiwatazama wajumbe 
 Msimamizi wa Uchaguzi wa viti Maalum udiwani jimbo la Shinyanga Mjini ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akisisitiza jambo kabla ya kuanza kwa zoezi la upigaji wa kura za maoni.
 Mmoja wa Wagombea wa nafasi ya udiwani akiwaomba wajumbe kumpigia kura ili aweze kuwasilisha  kero zao katika baraza la madiwani wa Manispaa ya Shinyanga akiwa amepiga Magoti kwa unyenyekevu.
 Mgombea akionyesha namba yake ya kupigiwa kura  huku wajumbe wakisubiri kufanya yao  na kupigia kura wanayeona ametoa sera za kuridhisha 
 Mgombea akiendelea kujinadi   na kubainisha sera zake kwa wajumbe 
 Miza Jilala Mgombea nafasi ya udiwani tarafa  ya Mjini Akiomba kura kwa wajumbe huku akionyesha  unyenyekevu ya kuwa licha ya  umri mdogo lakini ana uwezo wa kuwatumikia wanawake wa  Manispaa ya Shinyanga.
 Mmoja wa Wagombea ambaye ni mlemavu akiomba kupewa ridhaa ya kuwakilisha katika baraza la manispaa ya Shinyanga Mjini kupitia Kura za Wajumbe.
 Suzany Butondo mgombea wa Udiwani viti Maalum tarafa ya Mjini akiomba kura kwa wapiga kura huku akiinamisha kichwa  chini ishara ya kuwaangukia wajumbe wamfanyie wepesi katika kumpigia kura za maoni ambaye amebainisha kutatua kero zao.
  Wagombea wa Nafasi  ya Udiwani Viti Maalum Tarafa ya Ibadakuli Mshindi wa kwanza hadi wa tatu wakiwa wameketi pamoja na kuwashukuru wajumbe.
 Msimamizi akiwaambia jambo wajumbe na washindi wote baada ya kuhitimisha zoezi la kupiga kura za maoni 
 Washindi wa Kura za maoni wakifurahia kupitishwa na wajumbe 
  Zuhura Waziri akikumbatiana na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga aliyemaliza Muda wake Salome Makamba 


  Washindi wa Kura za Maoni Udiwani Viti Maalum Jimbo la Shinyanga mjini Wakiwa katika Picha ya Pamoja 
 Wagombea wakiendelea na Zoezi la kupiga Magoti 
  Mgombea aliyeshindwa kufikisha kura akiwashukuru wajumbe na wapiga kura 
  Mwenyekiti wa UWT-CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Bi Shambuo Katambi akiwashukuru wajumbe na wanachama wote kwa kuhitimisha zoezi katika mazingira salama

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post