NEC YATOA MAFUNZO YA SIKU TATU KWA WARATIBU WA MIKOA NA WASIMAMIZI WA UCHAGUZI MIKOA YA TANGA NA KILIMANJARO

 BAADHI ya waratibu wa uchaguzi wa mikoa,wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya Jimbo wakisaini fomu za viapo katika mafunzo ya siku tatu yanayoendelea shule ya Sekondari Galanosi Jijini Tanga
 Waratibu wa uchaguzi wa mikoa,wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya Jimbo wakisaini fomu za viapo katika mafunzo ya siku tatu yanayoendelea shule ya Sekondari Galanosi Jijini Tanga
 waratibu wa uchaguzi wa mikoa,wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya Jimbo wakisaini fomu za viapo katika mafunzo ya siku tatu yanayoendelea shule ya Sekondari Galanosi Jijini Tanga

 BAADHI ya waratibu wa uchaguzi wa mikoa,wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya Jimbo wakisaini fomu za viapo katika mafunzo ya siku tatu yanayoendelea shule ya Sekondari Galanosi Jijini Tanga


TUME ya Taifa ya uchaguzi NEC leo imeanza kutoa mafunzo ya siku tatu kwa waratibu wa mikoa na wasimamizi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi kwa mikoa ya Tanga na Kilimanjaro yenye lengo la kuwajengea uwezo wsatendaji hao ili waweze kutekeleza majuku yao kwa ufanisi katika uchaguzi mkuu Octoba 28 mwaka huu

Mafunzo hayo yameanza leo katika shule ya Sekondari Galanosi Jijini Tanga ambayo pia yanafanyika nchi nzima yakihusisha wasimamizi,wasimamizi wa uchaguzi na maafisa ugavi na maafisa uchaguzi kutoka majimbo 19 ya Tanga na Kilimanjaro.

Majimbo hayo kati yao 11 ni kutoka katika Mkoa wa Tanga na 8 ni kutoka katika mkoa wa Kilimanjaro ambao watakwenda kusimamia uchaguzi mkuu ambao utafanyika mwaka huu

Akizungumza wakati akifungua kikao cha wasimamizi wa uchaguzi mkuu ,Mkurugenzi Msaidizi wa Habari na Elimu ya Mpiga Kura NEC Dkt Cosmas Mwaisobwa kwa niaba ya Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo watendaji hao ili wanapokuwa wakitekelexa majukumu yao waweze kutekelexa kwa kadri inavtyotarajiwa kwa kuafuata taratibu zote.

Dkt Cosmas alisema kuwa pia ni kuhakikisha hawakumbana na changamoto ambazo zinaweza kuzuia utendaji wao kutokana na baadhi ya watendaji kuwa wapya walioteuliwa hivi karibuni huku wakiwa hawajapata uzoefu wa kusimamia uchaguzi wowote.

“Tunalenga kuwatumia wale ambao wana uwezo wa kusimamia uchaguzi kuwasaidia wenzao kubadilishana uelewa wa mambo yanayohusu usimamizi wa uchaguzi “Alisema Dkt Cosmas

Naye kwa upande wake Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Tanga Sebastian Masanja alisema wanawaelemisha kuhusu sheria mbalimbali zinazoongoza uchaguzi ambazo watazitumia wakati wakisimamia uchaguzi huo.

Masanja alisema lengo la mafunzo hayo ni kuandaa mchakato huru na haki kwa wadau wote wa uchaguzi leo wanawafundisha sheria mbalimbali zinazowaongoza kwa ajili uisimamiz wa uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Octoba mwaka huu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527