MAKADA 42 WA CCM WACHUKUA FOMU KUWANIA UBUNGE JIMBO LA TARIME MJINI NA TARIME VIJIJINI | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, July 15, 2020

MAKADA 42 WA CCM WACHUKUA FOMU KUWANIA UBUNGE JIMBO LA TARIME MJINI NA TARIME VIJIJINI

  Malunde       Wednesday, July 15, 2020
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI) ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Mwikwabe Waitara leo amechukua fomu ya kuomba kugombea Ubunge jimbo la Tarime vijijini.
 Nyerere Jackson Mwera akichukua fomu kugombea Ubunge Jimbo la Tarime mjini

Na Dinna Maningo - Malunde 1 blog Tar­ime.
Wanachama 42  wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamejitokeza kuchukua fomu za kuomba kugombea Ubunge Jimbo la Tarime mjini na Tarime vijijini kupitia CCM huku idadi ya wanawake ikiwa ndogo ikilinganishwa na wanaume. 


Akizungumza na Malunde 1 blog Katibu wa chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya  Tarime mkoani Mara,Hamis Mkaruka amesema kuwa hadi kufikia siku ya  leo Julai 15, 2020 wanawake waliochukua fomu ni watano pekee ,wana­ume wakiwa 37.

Mkaruka alisema kuwa kwa upande wa Jimbo la Tarime mjini wanawake  ni Suzy Chambili,Monica Anic­et na Dr.Veronica Robert ambapo Jimbo la Tarime vijijini ni Joyce Ryoba na Dr. Stella Faustine

Naye Naibu Waziri Of­isi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI) a­mbaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ukonga,M­wita Mwikwabe Waitara amechukua fomu ya kuomba kugombea Ub­unge jimbo la Tarime vijijini.

Makada wa CCM waliochukua fomu kuomba kugombea Ubunge hadi kufikia siku ya leo majira ya saa nane mchana waliochuk­ua fomu jimbo la Tar­ime vijijini ni 24 na Tarime mjini wakiwa 18 .

Wengine waliochukua fomu kwa jimbo la Tarime mjini ni Hezbon Mwera, Jackson Ryo­ba, Dr.Edward Machag­e,Julius Mtatiro Eng­.William Machage,Che­che Andrew,Julius La­baran,Samwel Marwa,E­vangel Otieno,Michael Kembaki,Jeremia Seba,Gerald Martine,M­wita Joseph,Zakayo Wangwe na Manchare He­che Siguta.

Kwa jimbo la Tarime vijijini ni Joseph Nyahende,Yusuph Wambu­ra,Chacha Masero,John Gimunta,Mwita Jacob Marwa,Wambura Sagi­re,Thomas Chacha Mwi­ta, Musa Raphael, Ny­erere Mwera,Nyamhanga David,Dr.Abdalah Chigo,Dr.Paul Mwikwab­e,Mordikae Moset,Eli­akimu Maswi,Nicodemas Keraryo,James Bwir­e,Peter Amos Bhusene Frank Mniko,Lucas Magoti,Samwel Mantarya na Ngocho Darius.

Katibu wa CCM wilaya ya Tarime Hamis Mka­ruka alisema kuwa wa­nawake wanapaswa kuo­ndoa hofu na badala yake wajitokeze kugo­mbea nafasi za Ubunge na Udiwani.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post