RAIS MAGUFULI: TANZANIA TUKO SALAMA NA WATALII WAMEANZA KUMIMINIKA....HONGERENI WIZARA YA MALIASILI | MALUNDE 1 BLOG

Monday, July 20, 2020

RAIS MAGUFULI: TANZANIA TUKO SALAMA NA WATALII WAMEANZA KUMIMINIKA....HONGERENI WIZARA YA MALIASILI

  Malunde       Monday, July 20, 2020

Rais Dkt John Pombe Magufuli, amesema kuwa Tanzania imebaki kuwa nchi salama, kwa kuwa ilifanikiwa kutokomeza mbali maambukizi ya Virusi vya Corona baada ya kumtanguliza Mungu na ndiyo maana hata watalii wameendelea kumiminika nchini kwa kuwa wanao uhakika na usalama wa maisha yao.


Rais Magufuli ametoa kauli hiyo hii leo Julai 20, 2020, wakati akizungumza na viongozi aliowateua mara baada ya kula viapo Ikulu ya Chamwino Jijini Dodoma.

"Wizara ya Maliasili nimeanza kuona watalii wengi wanakuja, kuna ndege zinaleta watalii wengi, watu wameangalia na wameuona ukweli kwamba hapa Tanzania tuko salama, maadui zetu watazungumza mengi, hata hapa tungekuwa tumevaa barakoa, lakini hakuna aliyevaa hapa ni kwa sababu tuko salama kwani sisi hatuogopi kufa?, lakini Corona iko mbali huko, tuliamua kumuomba Mungu na akatusikia" amesema Rais Magufuli.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post