GARI NNE ZAGONGANA PWANI | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, July 2, 2020

GARI NNE ZAGONGANA PWANI

  Malunde       Thursday, July 2, 2020

Gari nne yakiwemo malori mawili ya mafuta yamegongana na kusababisha ajali katika eneo la Mlandizi mkoani Pwani usiku wa kuamkia leo Julai 2,2020.

Ajali hiyo imetokea majira ya saa 5 Usiku wa jana Julai Mosi, na kupelekea kifo cha mtu mmoja na majeruhi watatu ambao wote wamekimbizwa katika Hospitali ya Tumbi.

Akithibitisha taarifa hiyo, Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Wankyo Nyigesa amemtaja marehemu kwa jina la Rahim Kurwa, huku akisisitiza kuwa abiria wanaotokea Dar es Salaam kwa kutumia barabara ya Morogoro watumie barabara ya Bagamoyo.

"Majeruhi wapo katika hospitali ya Tumbi pamoja na mwili wa marehemu lakini ninawashauri wasafiri wanaotokea Dar es Salaam watumie barabara ya Bagamoyo ili tuweze kuifungua hii barabara kwa sababu foleni ni kubwa sana", Kamanda Nyigesa

Credit: EATV


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post