LUCY MAYENGA ASHINDA KWA KISHINDO UCHAGUZI WA UBUNGE VITI MAALUM MKOA WA SHINYANGA | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, July 23, 2020

LUCY MAYENGA ASHINDA KWA KISHINDO UCHAGUZI WA UBUNGE VITI MAALUM MKOA WA SHINYANGA

  Malunde       Thursday, July 23, 2020

Kulia ni Lucy Mayenga akihesabu kura zake.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Lucy Mayenga ameshinda kwa kishindo uchaguzi wa kura za maoni

UWT mkoa wa Shinyanga kwa kupata kura 277 kati ya kura 335 zilizopigwa huku Kirumba Santiel Erick akishika nafasi ya pili kwa kupata kura 155 na Mnzava Christina Christopher akishika nafasi ya tatu baada ya kupata kura 109.Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika leo Alhamis Julai 23,2020 katika Ukumbi wa CCM mkoa wa Shinyanga,na kuhudhuriwa na Wajumbe wa mkutano mkuu UWT Mkoa wa Shinyanga, Msimamizi wa uchaguzi Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack amewapongeza akina mama wote kwa kuingia kwenye kinyang'anyiro na kuwataka kuwa wamoja ili kupata ushindi katika uchaguzi mkuu.

"Kulikuwa na wagombea 42 lakini sisi tunahitaji watatu. naomba msiwe na kinyongo twende sasa tuwe timu moja tufanye kazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).Kwa sasa tubaki timu moja ya mkoa wa Shinyanga, akina mama tukiungana hatuwezi kupoteza kura hata moja",amesema Telack.
Hata hivyo Mkuu huyo wa mkoa aliwataka wajumbe wa mkutano huo kuvunja makundi walivyokuwa nayo wakati wa mchakato wa uchaguzi huku akiwataka wale wenye malalamiko kuwasilisha malalamiko yao kwa maandishi ndani ya siku tatu.
Msimamizi wa Uchaguzi wa Kura za maoni Ubunge Viti Maalum ambayeMkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi Zainab Telack akitangaza matokeo ya uchaguzi. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Msimamizi wa Uchaguzi wa Kura za maoni Ubunge Viti Maalum ambayeMkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi Zainab Telack akitangaza matokeo ya uchaguzi
Wajumbe wa mkutano wakiwa ukumbini.
Mmoja wa wagombea akiomba kura kwa wajumbe
Wagombea ubunge Viti maalum wakiwa ukumbini
Wagombea ubunge Viti maalum wakiwa ukumbini
Wagombea ubunge Viti maalum wakiwa ukumbini
Wajumbe wa mkutano wakiendelea na zoezi la upigaji kura
Wajumbe wa mkutano wakiendelea na zoezi la upigaji kura
Wajumbe wa mkutano wakiendelea na zoezi la upigaji kura
Wajumbe wakiwa ukumbini.

Wagombea wakiwa ukumbini.
Wagombea wakiwa ukumbini.
Wajumbe wakichukua karatasi za kupigia kura
Mjumbe akipiga kura
Zoezi la kupiga kura likiendelea.
Zoezi la kuhesabu kura likiendelea.

Zoezi la kuhesabu kura likiendelea. Kulia ni Lucy Mayenga akihesabu kura zake.

Zoezi la kuhesabu kura likiendelea.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post