WAZIRI WA MAJI PROFESA MAKAME MBARAWA AJITOSA KUGOMBEA URAIS ZANZIBAR


Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa,  amechukua fomu ya kuwania urais Zanzibar katika uchaguzi mkuu mwezi Oktoba kupitia Chama cha Mapinduzi CCM.


Mbarawa amekuwa mwanachama wa kumi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) aliyejitosa kuchukua fomu kuwania Urais wa Zanzibar kupitia chama hicho

Profesa Mbarawa amekabidhiwa  fomu hizo leo Ijumaa tarehe 19 Juni 2020 na Cassian Gallo’s,  Katibu wa Kamati Maalumu ya NEC idara ya Oganaizesheni Zanzibar katika Ofisi za CCM Kisiwandui, Ugunja Zanzibar.

Baada ya kukabidhiwa fomu hiyo, Profesa Mbarawa, amewaomba Wazanzibar na Watanzania kumuombea kwa Mungu, ili akamilishe taratibu zinazofuata salama, ikiwemo utafutaji wadhamini 250 katika mikoa mitatu ya Zanzibar.

“Natamani nifanye hivyo (kuongea kuhusu sababu za kutia nia ya kugombea urais), lakini naomba leo tusiongee mengi sababu ninakwenda kazini,  tuombe Mungu atufikishe salama. Ninalowaomba tumuombe Mungu atusimamie, atufanyie wepesi,” amesema Prof. Mbarawa.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527