MWANAMAMA MWATUM SULTAN ACHUKUA FOMU KUGOMBEA URAIS ZANZIBAR | MALUNDE 1 BLOG

Friday, June 19, 2020

MWANAMAMA MWATUM SULTAN ACHUKUA FOMU KUGOMBEA URAIS ZANZIBAR

  Malunde       Friday, June 19, 2020

Na Andrew Chale -  Zanzibar
Kwa mara ya kwanza Kada wa CCM, Mwanamama, Mwatum Mossa Sultan leo Juni 19,2020 amechukua fomu za kutaka kuteuliwa nafasi ya Mgombea wa Urais wa Zanzibar ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kufanya idadi ya makada waliojitokeza hadi leo kuwa 11.

Mwanamama huyo alipata fursa ya kuongea na wanahabari ambapo amesema lengo ni kuongeza hamasa kwa akina mama wengine nao wajitokeze.

"Namuomba Mungu anipe subra. Aniongoze katika safari yangu hii ndefu. Mimi ni Kada wa CCM na nina uzoefu mkubwa katika chama",alisema Mama Mwatum.

Wengine waliochukua fomu Ofisi Kuu ya CCM-Zanzibar zilizopo Kisiwandui, ni pamoja na Waziri wa Maji wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Profesa Makame Mbarawa, Shamsi Vuai Nahodha, Mohammed Jafari Jumanne, Mohammed Hija Mohammed,Balozi Meja Jenerali Mstaafu, Issa Suleiman Nassor, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Kwahani Mjini Unguja, Zanzibar, Mbwana Bakari Juma, Balozi Ali Karume, Mbwana Yahaya Mwinyi na Omary Sheha Mussa.

Tukio la kukabidhiwa fomu linatarajiwa kufungwa rasmi 30 Juni huku likisimamiwa na Katibu wa Idara ya Organization CCM, Zanzibar, Cassian Galos.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post