KITABU CHA NIMEJITAKIA CHA MOHAMMED HAMMIE CHAZINDULIWA RASMI


Mwandishi wa Kitabu cha NIMEJITAKIA Bwana Mohammed Hammie Rajab akiwa katika duka la vitabu la TPH lililopo posta.
***
Hatimae kitabu cha NIMEJITAKIA kilichoandikwa na Mohammed Hammie kilichokuwa kikisubiriwa kwa hamu na wasomaji wa riwaya nchini Tanzania na Afrika Mashiriki kimetoka rasmi huku kikipokelewa kwa bashasha fasihini.

Akizungumza nasi mwandishi wa kitabu hicho Bwana Mohammed amesema kuwa tayari riwaya hiyo imeshaanza kusambazwa katika baadhi ya maeneo hapa nchini ambapo kwa mkoa wa Dar es salaam kinapatika katika duka la TPH Bookshop lililopo posta, duka la kona ya riwaya lililopo Moroko, pamoja na muuza vitabu maarufu eneo la Posta anayejulika kwa jina la George ambaye yupo katika makutano ya barabara ya Samora, au kwa kupiga nambari 0625634902 unaletewa popote kwa wakazi wa Dar es salaam huku kwa mikoa ambayo bado kitabu hakijafika unatumiwa.

Mikoa mengine inayopatikana kitabu hicho ni Arusha kupitia nambari ya simu: 0757690302, Morogoro kwa nambari ya simu 0659601522, huku mikoa kama Dodoma, Tanga na Mbeya ikitarajiwa kupokea kitabu hicho hivi karibuni.

Kitabu cha NIMEJITAKIA ambacho kimehaririwa na Bi Laura Pettie na kuhakikiwa na Mariam Mbano ni simulizi inayomhusu kijana Issa Matone. Kijana aliyefadhiliwa kisha kumlipa ubaya mfadhili wake.

Kijana huyo alipoamua kulichuma janga, hakutarajia janga hilo lingemshikia kiboko na kumcharaza vibaya mno. Lakini kitabu kinaonyesha namna Issa alivyoonywa, ila hakusikia. Hivyo yaliyomkuta, ni kama alijitakia. Ni simulizi yenye mafunzo lukuki ndani yake.

Katika kuhakikisha wasomaji nchini kote wanafikiwa na kujifunza kutoka katika Kitabu cha NIMEJITAKIA menejimenti ya mwandishi Mohammed Hammie imeandaa shindano lililopewa jina la Jitakie Na Ushinde lililozinduliwa rasmi leo kupitia mitandao ya kijamii hususani Facebook,unaweza kujua zaidi kuhusu shindano hilo kwa kutembelea kurasa za mtandao wa kijamii wa facebook kwenye ukurasa wa mwandishi Laura Pettie,Mariam Mbano,Hanifa Kafashe au mwandishi mwenyewe .

Hii ni riwaya ya pili kutoka kwa mwandishi Mohammed Hammie Rajab, riwaya yake ya kwanza ni ile ya YALIYONIKUTA TANGA, ambayo bado inafanya vizuri sokoni.

Mohammed ni mtoto wa aliyekuwa nguli wa uandishi nchini Tanzania, marehemu Hammie Rajab aliyewahi kutamba na riwaya kama Sanda Ya Jambazi, Kamlete Akibisha Mlipue, Somo Kaniponza, Ama Zangu Ama Zao, Balaa na nyengine nyingi.

Kwa shilingi 10,000/= tu za Kitanzania unajipatia kitabu cha NIMEJITAKIA ukajifunza na kuburudika vya kutosha.
Mohammed Hammie aliyesimama katikati akiwa na Bi Hanifa Kavashe aliyevaa blauzi nyeusi na Bi Mariam Mbano wakati wa uzinduzi wa kitabu cha NINEJITAKIA.
Mohammed akiwa na mdau vitabu na msomaji mashuhuri hapa nchini Bwana Salim Aljabry. 
Mohammed Hammie akiwa na mwandishi nguli wa riwaya hapa nchini Bwana Hussein Issa Tuwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527