WAJUMBE SITA CCM WALIOSIMAMISHWA KWA TUHUMA ZA RUSHWA ZANZIBAR WAREJESHWA KAZINI

Na Faustune Gimu,Dodoma

MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa (UVCCM), HERI JAMES ametangaza kuwa jumuiya hiyo inawarejesha  kazini  wajumbe sita wa umoja huo Zanzibar  waliokuwa wakituhumiwa  kwa kosa la kutoa na kupokea rushwa.

Akizungumza jana jijini Dodoma na waandishi wa habari Mwenyekiti huyo amesema  uamuzi huo ni baada ya uchunguzi uliokuwa ukifanywa na Mamlaka ya Kuzuia  Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar (ZAECA) kukamilika na kukutwa hawana hatia.

Amewataja wajumbe hao kuwa ni Pandu salum Sungura, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kaskazini Unguja, Amina Bakari Yusuph Mjumbe wa Baraza kuu la UVCCM Mkoa wa Kaskazini Unguja, Alawi Hadali Faumu Katibu wa UCCM Mkoa wa Kaskazini Unguja, Fransisca Clement Mjumbe Baraza Kuu la UVCCM Mkoa wa Mjini , Hussein Ayub Idd ,Mjumbe Baraza Kuu la UVCCM Mkoa wa Mjini Lulu Mwacha Mjumbe Baraza Kuu la UVCCM Mkoa wa Arusha.

“Tulifanya maamuzi ya kuwasimamisha wajumbe hawa kupitia kamati ya utekelezaji kutokana na tuhuma zilizoibuliwa za kutoa  na kupokea rushwa sasa leo ninavyozungumza taasisi ya ZAECA imewasiliasha taarifa rasmi kwa Chama Cha Mapinduzi kwamba vijana hawa hawakuhusika nataka niwaombe vijana wa CCM katika hili hatuna mzaha yeyote atakayebainika akifanya vitendo hivi tutamchkulia hatua kama watu wengine bila ubaguzi” Amesema.

Aidha,ameipongeza ZAECA na jeshi la polisi  kwa kufanya majukumu yake kwa weledi bila upendeleo pamoja na pongeza vijana hao kwa utulivu waliokuwa nao wakati wote wa kusimamishwa kwao akiwatka wanaporudi katika majukumu yao kuwa na ari ya kufanya kazi kwa uaminifu kwa manufaa ya Chama na Taifa kwa ujumla.

Sanjari na hayo amesikitishwa na taabia ya baadhi ya watu kuwafanyia vitendo vya udhalilishaji na kejeli kwa baadhi ya wagombea waliojitokeza kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali kutokana na jinsia zao au kwa sababu aliwahi kushika nafasi katika taasisi za umma akisema kwamba kugombea ni haki ya kila mtanzania kwa mujibu wa katiba ya nchi.

“Kumekuwa na siasa za kuwatweza, kuwashutumu kwasabau tu wamewahi kuwa viongozi wa umma huko Zanzibar na sababu nyingine niseme kugombea ndani ya Chama cha mapinduzi niwakumbushe watanzania suala la kugombea haki ya kikatiba kwa kila raia haijalishi aliwahi kuwa nani, wapi na kwa maslahi gani na kugombea kwa chama chetu pia ni haki  ila vikao vitu tutavitumia kuchambua nani anafaaa kwa wakati huo.”amebainisha.

Hivyo,amewataka  vijana wa CCM kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mabalimbali ikiwemo udiwani katika meneo yao akisema kwamba vijana ni jeshi kubwa lenye nguvu hivyo ni wakati wao sasa kuonyesha uwezo wao kwa manufaa ya wananchi  an akwamba maendeleo yapo mikononi mwa vijana.

“Sasa hivi tunajiandaa na uchaguzi mkuu na tayari fomu zimeanza kuchukuliwa vijana mna nafasi kubwa sana jitokezi mchukue fomu mbna mna uwezo mkubwa huna haja ya kuhofia sijui kipato uwezo wako ndio utakaokubeba na hata ikitokea hujapata nafasi basi shikirikiana na waliopata tuijenge nchi yetu” Amesema.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527