MKURUGENZI WA TAMWA AWATAKA WANAWAKE WAJASIRIAMALI KUTUMIA VIZURI NEEMA YA ZAO LA KARAFUU
Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake TAMWA-Zanzibar Dkt,Mzuri Issa (katika) akitazama baadhi ya bidhaa zinazozalishwa na wajasiriamali Kisiwani Pemba,kulia ni Asha Mussa Afisa uwezeshaji uchumi TAMWA ofisi ya Pemba kushoto ni Sakina Bakari Ame.

Na Muhammed Khamis-TAMWA-Zanzibar

Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake TAMWA- Zanzibar Dkt,Mzuri Issa amewataka wanawake wajasiriamali Kisiwani Pemba kutumia vizuri neema ya zao la karafuu kisiwani humo kwa kuzalisha bidhaa mbalimbali.

Dkt Mzuri aliyasema hayo leo wakati alipokuwa akikagua baadhi ya bidhaa zinazozalishwa na wajasirimali hao kutoka Pemba ofisini kwake Tunguu Wilaya ya kati Unguja.

Alisema zao la karafuu linaweza kuzalisha bidhaa mbali mbali ambazo zina soko kubwa ndani na je ya nchi iwapo wajasiriamali hao wataweza kuzisanifu vyema karafuu hizo.

Akitolea mfano wa bidhaa zinazotokana na karafuu alisema ni sabuni pamoja na liwa ambalo ni maalumu na hutumika kwa ajili ya kusafishia mwili kwa wanawake na wanaume (singo)

Pia Dkt, Mzuri aliwataka wajasiriamali hao kuanza kuangaza zaidi soko la kimataifa ambapo pia kuna uhitaji mkubwa wa bidhaa za asili kutoka Zanzibar hususani zinazoalishwa kwa kutumia karafuu na mengineyo.

Kwa upande wake Afisa Uwezeshaji Wanawake TAMWA ofisi ya Pemba Asha Mussa alisema wanawake wengi kisiwa cha Pemba wamehamasika na kujiunga kwenye vikundi mbali mbali vya uzalishaji wa bidhaa.

Akitolea mfano alisema pia wajasiriamali hao hawakuridhika tu na
uzalishaji wa bidhaa hizo pia wameanza kujiungiza katika ufuagaji ambapo tayari baadhi ya vikundi vinamiliki mabanda ya na wanaendelea na ufugaji kuku.

Akizungumzia kuhusu changamoto alisema bado zipo changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa soko la uhakika kwa wajasiriamali ambapo wakati mwingine wajasirimali hao hulazimika kukaa na bidhaa zao ndani kwa muda mrefu.

Afisa huyo uwezeshaji wanawake kiunchumi aliomba Serikali na taasisi nyingine mbali ndani ya Zanzibar na nje ya Tanzania kujitokeza kwa wingi kuunga mkono jitihada za vikundi hivyo kwa kuwa kufanya hivyo kutawawezesha wanawake wengi kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umaskini.

Akizungumzia kuhusu hali halisi ya uzalishaji wa bidhaa mmoja miongoni mwa wajasiriamali kutoka kisiwani Pemba Sakina Ame Bakar alisema wanajitahidi katika uzalishaji wa bidhaa bora na zenye viwango vya hali ya juu.

Alisema licha ya jitihada hizo lakini wanaendelea kukabiliwa na changamoto ya ukosefu wa soko bora na lenye uhakika kwao ambalo lingewafanya kwa wajasiriamali bora na wa kimataifa.

Aidha aliomba Serikali kuendelea kuwatengezea mazingira ikiwemo kuwakutanisha na makampuni makubwa pamoja na wajasiramali wengine wa kimataifa ili waweze kutengeza masoko mapya.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527