NAIBU SPIKA DKT TULIA ACKSON AKIWASILI HOSPITALI KUMJULIA HALI FREEMAN MBOWE ALIYEVAMIWA NA KUVUNJWA MGUU DODOMA | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, June 9, 2020

NAIBU SPIKA DKT TULIA ACKSON AKIWASILI HOSPITALI KUMJULIA HALI FREEMAN MBOWE ALIYEVAMIWA NA KUVUNJWA MGUU DODOMA

  Malunde       Tuesday, June 9, 2020

Naibu Spika, Dkt Tulia Ackson akiwasili katika Hospitali ya DCMC Ntyuka kumjulia hali M/Kiti wa Chadema na Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe aliyelazwa katika hospitali hiyo akipatiwa matibabu baada ya kuvamiwa na kujeruhiwa na watu wasiojulikana.


*****

Naibu Spika, Dk.Tulia Ackson  amemjulia hali Mwenyekiti Chadema, Freeman Mbowe katika Hospitali ya Ntyuka, Dodoma anakopatiwa matibabu  baada ya kuvamiwa na watu wasiojulikana na kisha kujeruhiwa na kuvunjwa mguu mmoja na kusema kuwa amemuona akiwa na majeraha mguuni na kwamba wanasubiri taarifa ya daktari ili kujua ameumia kwa kiasi gani.

"Ana maumivu ya mguu, mimi nimemuona ila bado wanaendelea kufanya uchunguzi na vipimo vingine, niwatoe hofu watanzania kwamba yupo anaendelea kupata huduma"- Amesema Naibu Spika Baada ya kumtembelea Mbowe 


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post