BIBI WA MIAKA 65 AFUNGA NDOA NA MTOTO WAKE WA MIAKA 24 | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, June 16, 2020

BIBI WA MIAKA 65 AFUNGA NDOA NA MTOTO WAKE WA MIAKA 24

  Malunde       Tuesday, June 16, 2020

Wanandoa Mbah Gambreng (65) na mumewe Ardi Waras (24)

Bibi wa miaka 65 aliyetambulika kwa jina la Mbah Gambreng amekubali kufunga ndoa na mwanaye wa kumnunua au kufikia aitwaye Ardi Waras mwenye miaka 24 huko Kusini mwa Sumatra nchini Indonesia.

Bibi huyo amesema walikuwa wanaishi pamoja tangu mwaka jana kipindi alipokuwa mtoto wake wa kiume, na hadi sasa ameamua kuolewa naye baada ya kuingia kwenye mahusinao, na hakutegemea kama angeweza kuchumbiwa na kufunga naye ndoa.

Aidha mzee huyo ambaye anamiliki watoto wengine watatu wa kike wa kufikia na kuwanunua ameongeza kusema, alipata mshangao baada ya kuambiwa anataka kuolewa na mtoto wake huyo.

Mtoto wake huyo ambaye amemuoa anadaiwa alilipa mahari ya Rupia 100,000 kwa pesa ya Indonesia sawa na Tsh 16,396, pia wanandoa hao walishea picha zao kwenye mitandao ya kijamii huku wakiwa wameshikana mikono na kila mmoja akifurahia kampani ya mwenzake.

Uwepo wa umri kati ya mzee huyo na mwanaye haimaanishi kama ndiyo ndoa ambayo wamezidiana kwa umri mrefu, kwani mnamo mwezi Februari mzee wa miaka 100 alimuoa binti wa miaka 20 na kupishana tofauti ya miaka 80 hukohuko nchini Indonesia.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post