TANZANIA YATAJWA KUWA NCHI YA KWANZA KWA UTULIVU NA AMANI KATIKA UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI


Tanzania imetajwa kuwa nchi ya kwanza kwa utulivu na amani katika Ukanda wa Afrika Mashariki, pia imeshika nafasi ya saba katika nchi zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara.


Kauli hiyo ameitoa leo tarehe 16 Juni 2020,  na Rais Magufuli jijini Dodoma wakati akifunga Bunge la 11 kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kutoa fursa mchakato wa uchaguzi mkuu kuanza.

Amesema, wakati akiingia madarakani kulikuwa na wimbi kubwa la uhalifu wa kutumia silaha na mauaji jambo ambalo vikosi vya ulinzi na usalama limesimamia na kumaliza matukio hayo.

“Ripoti ya Global Peace Index 2020 imeitaja Tanzania kushika nafasi ya kwanza kwa amani na utulivu kwenye eneo la Afrika Mashariki, na nafasi ya saba kwa nchi zilizoko Kusini mwa Jangwa la Sahara, kwa niaba ya Watanzania wote navipongeza vyombo vya ulinzi na usalama kwa kazi kubwa.

“Wakati tukiingia madarakani, kulikuwa na wimbi kubwa la uhalifu wa kutumia silaha, pamoja na matukio ya mauaji kule Kibiti na kupitia Vyombo vya Ulinzi na Usalama vitendo hivyo vilikomeshwa na nipende kusema kuwa nchi yetu kwa sasa ni salama,” amesema Rais Magufuli.

Amesema, wakati akiingia madarakani, miongoni mwa ahadi yake katika utawala wake ni kudumisha amani na mshikamano ambavyo sasa vimeshuhudiwa nchini.

“Mojawapo ya ahadi kubwa niliyoitoa wakati wa kuzindua Bunge ni kudumisha amani, umoja, mshikamano, ninayo furaha kuwa tumetimiza ahadi hiyo kwa vitendo kwani Watanzania tumeeendelea kuwa wamoja na kushirikiana.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527