NAIBU WAZIRI WA AFYA DKT.MOLLEL ATEMBELEA BOHARI YA DAWA (MSD) DAR ES SALAAM

Na WAMJW- DSM.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt Godwin Mollel ametembelea Bohari ya Dawa (MSD) Makao Makuu na kuzungumza na watumishi wa taasisi hiyo ili kufahamu namna taasisi hiyo inavotekeleza majukumu yake.

Akizungumza na viongozi wa Bohari ya Dawa Jijini Dar es Salaam Dkt Mollel amesema lengo la kutembelea taasisi hiyo ni kuangalia maboresho katika uagizaji, utunzaji na usambazaji wa dawa vifaa tiba na vitendanishi vya maabara ili kuboresha huduma ya afya nchini.

Amesema maboresho hayo ni njia ya kuelekea mafanikio ya pamoja katika kutatua changamoto za wananchi hususani katika upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara.

Kwa upande wake mtendaji mkuu wa MSD Maja Jenerali Gabriel Saul Mhidze (Dkt) amesema ujio wa naibu waziri umeongeza chachu katika utekelezaji wa majukumu ya taasisi kiujumla pamoja na utekelezaji wa maelekezo yanayo tolewa na wizaya ya afya ili kuendana na kasi inayohitajika katika sekta ya afya.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527