NTOBI AJITOSA UBUNGE SHINYANGA MJINIAliyekuwa Diwani wa Kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga (2015-2020) ambaye sasa ni Mwenyekiti wa Umoja wa Madiwani CHADEMA Kanda ya Serengeti mkoa wa Simiyu Mara na Shinyanga, Emmanuel Ntobi ametangaza nia ya kugombea ubunge katika Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Ntobi ametangaza leo Jumamosi Juni 27,2020 kuanza mbio za kuusaka ubunge kupitia CHADEMA akieleza kuwa atashukuru endapo Chama chake kitampa ridhaa ya kuwa mgombea Ubunge katika uchaguzi  Mkuu wa Tanzania mwaka 2020.

"Naamini katika nguvu na mamlaka ya umma 'The People's Power' katika kumiliki, kuendesha,kubuni na kuendeleza maamuzi,mawazo,rasilimali,uchumi na siasa yetu. Shinyanga Deserves Better",amesema Ntobi.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527