Picha : TAKUKURU SHINYANGA YAWAPIGA MSASA WANACHUO RUSHWA YA NGONO...WENYEWE WASEMA TATIZO "MAKSI ZA BURE"




Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) mkoani Shinyanga, imetoa elimu ya rushwa ya ngono kwa wanavyuo mkoani Shinyanga kwa ajili ya kutokomeza vitendo hivyo.


Elimu hiyo imetolewa leo Juni 27, 2020 katika Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Mkoani Shinyanga, na kukutanisha wanachuo kutoka  Chuo cha VETA, Chuo cha Ualimu (Shycom), pamoja na wenyeji wa chuo hicho cha Ushirika.

Akitoa elimu hiyo mkuu wa TAKUKURU mkoani Shinyanga Hussein Mussa, amesema wametoa elimu hiyo ya rushwa ya ngono wa wanachuo, eneo ambalo wanafunzi wake hasa wa kike ndiyo wamekuwa wahanga wakubwa wa matukio hayo, kutokana na hatima ya ufaulu wao kuwa mikononi mwa wahadhiri.

Amesema katika mkoa wa Shinyanga tangu wazindue dawati la Rushwa ya ngono mwaka jana (2019), wameshapokea taarifa mbili za wanachuo kuombwa rushwa ya ngono, ambapo kesi zake bado zinaendelea, na kutoa wito kwa wanachuo wasiwe wasiri bali watoe taarifa kwa wingi pale wanapoombwa rushwa ya ngono na wahadhiri wao.

“TAKUKURU inatoa elimu hii ya rushwa ya ngono nchi nzima, na sisi tumeamua hapa mkoani Shinyanga tutoe elimu hii kwa wanachuo wetu ambao ndiyo wahanga wakubwa, ili tuwe kitu kimoja kutokomeza vitendo hivi kwa kupewa taarifa,” amesema Mussa.

Naye Kaimu Mratibu wa Mafunzo kutoka Chuo cha ushirika Moshi tawi la Kizumbi Mkoani Shinyanga Samson Charles, amesema rushwa ya ngono kwenye vyuo ipo, isipokuwa kuna usiri mkubwa ambao unatawala, kutokana na mwanchuo kutaka apatiwe maksi za bure ili apate ufaulu mzuri kwa sababu ya uzembe wake wa kujisomea.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Klabu ya wapinga rushwa chuoni hapo Kombeho Wiliam, amewataka wanachuo wajikite kwenye masomo, na siyo kusubiri kupewa maksi za bure kwa kutoa rushwa ya ngono, jambo ambalo litasababisha nchi kupata viongozi wasio na maadili na wasio na uwezo wa kuchapa kazi sababu ufaulu wao unatokana na rushwa.



TAZAMA PICHA HAPA CHINI


Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Shinyanga Husseni Mussa akitoa elimu ya rushwa ya ngono kwa wanafunzi kutoka  Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Mkoani Shinyanga, Chuo cha VETA na Chuo cha Ualimu (Shycom) leo Jumamosi Juni 27,2020. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde 1 blog

Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Shinyanga Hussen Mussa, akiwataka wanachuo mkoani humo watoe taarifa pale wanapokuwa wakiombwa rushwa ya ngono na wahadhiri wao.

Kaimu Mratibu wa mafunzo kutoka Chuo cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Mkoani Shinyanga Samson Charles, akiwataka wanachuo na wahadhiri mkoani humo waachane kabisa na vitendo vya rushwa ya ngono.

Mwenyekiti wa klabu ya wapinga rushwa kutoka chuo cha ushirika Moshi tawi Kizumbi Mkoani Shinyanga Kombeho Wiliam, akiwataka wanachuo wajitambue na kusoma kwa bidii na siyo kusubiri maksi za bure kwa kutoa rushwa ya ngono.

Wanachuo wakisikiliza elimu ya rushwa ya ngono kutoka TAKUKURU.

Wanachuo wakiendelea kusikiliza Elimu ya rushwa ya ngono.

Wanachuo wakiendelea kusikiliza Elimu ya rushwa ya ngono.

Wanachuo wakiendelea kusikiliza Elimu ya rushwa ya ngono.

Wanachuo wakiendelea kusikiliza Elimu ya rushwa ya ngono.

Mwanafunzi kutoka Chuo cha Ualimu (Shycom) Rahel Ezekiel, akichangia mada wakati wa majadiliano.

Mwanafunzi kutoka VETA Chausiku Ipini , akichangia mada wakati wa majadiliano.

Mwanachuo kutoka Chuo cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi mkoani Shinyanga Betina Mwashambwa, akichangia mada wakati wa majadiliano.

Mkuu wa TAKUKURU mkoani Shinyanga Hussen Mussa, (mwenye kaunda suti katikati), akipiga picha ya pamoja na wanachuo mara baada ya kumaliza kutoa elimu ya rushwa ya ngono.

Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527