MWANACHUO AMUUA MWENZAKE KWA KISU WAKIGOMBANIA MWANAFUNZI CHUMBANI | MALUNDE 1 BLOG

Friday, June 26, 2020

MWANACHUO AMUUA MWENZAKE KWA KISU WAKIGOMBANIA MWANAFUNZI CHUMBANI

  Malunde       Friday, June 26, 2020
Mwanafunzi wa Chuo cha Utumishi Kange, mkoani Tanga aitwaye Waziri Ramadhan anadaiwa kumuua mwanafunzi mwenzake aliyejulikana kwa jina la Athumani Ally Daudi  kwa kumchoma kisu baada ya kumkuta kwenye chumba cha rafiki yake wa kike.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Kamishna Msaidizi, Blasius Chatanda, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kueleza kuwa palitokea ugomvi baina ya wanafunzi wa kiume.

Ugomvi huo ulizuka juzi, baada ya kukutana kwenye chumba cha msichana huyo, huku kila mmoja akiona kuwa ana haki ya kummiliki msichana huyo.

Kwa mujibu wa Kamanda Chatanda, aliyefariki dunia katika tukio hilo ni Athumani Ally Daudi, ambaye anadaiwa alichomwa kisu na Waziri Ramadhan.

Kamanda huyo alisema wanamshikilia binti huyo, huku mtuhumiwa akidaiwa kukimbia.Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post