Mahakama Ya Katiba Burundi Yaagiza Rais Mteule Aapishwe Haraka Baada ya Kifo cha Pierre Nkurunziza | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, June 13, 2020

Mahakama Ya Katiba Burundi Yaagiza Rais Mteule Aapishwe Haraka Baada ya Kifo cha Pierre Nkurunziza

  Malunde       Saturday, June 13, 2020
Mahakama ya kikatiba ya Burundi imeamua kuwa rais mteule Meja Jenerali mstaafu Evariste Ndayishimiye aapishwe urais mara moja na hakutakuwa na rais wa mpito..

Katiba ya nchi hiyo inaeleza kuwa spika wa bunge atatakiwa kuchukua nafasi hiyo kwa mpito pale rais anapofariki. 

Hata hivyo Mahakama ya Katiba iimeamua kwamba kutokana na hali inayojiri kwa sasa, "hakuna ulazima wa kuwepo na rais wa mpito". Hoja kuu ya Mahakama ni kuzingatia kwamba madhumuni ya serikali ya mpito - ambayo ni kuandaa uchaguzi wa mapema iwapo kutakuwa na ombwe la uongozi nchini - hoja ambayo haipo tena nchini Burundi '' baada ya kuepo na rais mteule.

Wakati huo Mahakama ya Katiba imeagiza kwamba Jenerali Evariste Ndayishimiye aapishwe "haraka iwezekanavyo" ili kuchukuwa hatamu ya uongozi wa nchi.

Hukumu hii ya Mahakama ya Katiba inamaliza sintofahamu iliyokuepo kuhusu nani atakaye chukuwa nafasi ya rais baada ya rais Pierre Nkurunziza kufariki dunia ghafla Jumatatu Juni 8 kuokana na "shinikizo la moyo" kwa mujibu wa serikali ya Burundi.

Ndayishimiye wa chama tawala cha CNDD-FDD aliyechaguliwa Mei 20 awali ilikuwa aapishwe mwezi Agosti.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post