JAMAA AKAMATWA KWA KUBAKA WANAWAKE 40

Polisi nchini Nigeria wamemkamata mtu wanayedai kuwa amewabaka wanawake 40 katika mji mmoja katika kipindi cha mwaka mmoja.

Kwa mujibu wa msemaji wa polisi Abdullahi Haruna, mtu huyo alikamatwa baada ya mwanamke mmoja katika mji wa Dangora kaskazini mwa Nigeria kumpata akiwa amejificha katika chumba cha watoto kulala.

 Bw. Haruna aliongeza kuwa mtu huyo alijaribu kutoroka lakini majirani walimkimbiza na kumshika.

Kumeshuhudiwa msururu wa ubakaji na mauaji ya wanawake katika siku za hivi karibuni Nigeria, hali ambayo imesababisha hasira miongoni mwa wananchi, huku maelfu yao wakitia saini ombi la kupinga uovu huo na kutaka hatua zichukuliwe kwa kutumia hashtag #WeAreTired.

Dangora ni mji mdogo katika jimbo la Kano karibu kilomita 85 kusini -magharibi mwa jimbo hilo, hali ambayo inawafanya polisi kutofika kwa muda unaostahili, anasema mwandishi wa BBC Mansur Abubakar kutoka Kano.

Chifu kiongozi wa mji huo, Ahmadu Yau, alisema kukamatwa kwa mshukiwa huyo ni hatua muhimu kuelekea kukabiliana na uhalifu huo.

"Watu wa Dangora wanafurahia sana hatua zilizochukuliwa na tunatumaihaki ya itatekelezwa."

Wakaazi waliambia BBC kwamba mwaka jana waliishi kwa uwoga,hata ndani ya nyumba zao, kwa sababu walidokezewa wabakaji wanaruka ua na kuingia majumbani kuwabaka wanawake.

"Sasa tunaweza kufunga macho na kulala kwa amani," mmoja wa wanawake aliambi BBC.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post