JAMAA AJISALIMISHA POLISI AKIWA UCHI BAADA YA KUFUMANIWA AKIHONDOMOLA MKE WA MWANAJESHI


Mwanaume aliyefumaniwa akiwa kituo cha polisi 

Mwanaume mmoja nchini Kenya amejisalimisha kituo cha polisi cha Embakasi Jijini Nairobi akiwa hana nguo baada ya kukimbia kutoka kwenye fumanizi nyumbani kwa mke wa Mwanajeshi.

Jamaa huyo alifika katika Kituo Cha Polisi cha Embakasi, usiku wa Jumamosi, Juni 13,2020 kutafuta ulinzi dhidi ya afisa wa Jeshi ya Ulinzi ya Kenya (KDF) ambaye alikuwa anamkimbiza.

Imeelezwa kuwa mume wa mwanamke huyo ambaye ni Mwanajeshi alirudi ghafla nyumbani bila taarifa na kumkuta mkewe na mwanaume huyo wakiwa ndani, ndipo alipofanikiwa kukimbia. 

Alifika kituoni akiwa mwenye wasiwasi mkubwa huku akiomba msaada wa kuokolewa dhidi ya mume wa mwanamke aliyekutwa naye, ambaye alikuwa anamtafuta kila mahali. 

Akiandikisha taarifa katika kituo cha polisi, mwanaume huyo aliyefumaniwa amesema kuwa mwanamke alimuambia kuwa ni mjane, baada ya mumewe kufariki dunia katika shambulio la Dusit D2 mwaka uliopita.

Kulingana na mwanamume huyo, mpenzi wake alikuwa amemuarifu kwamba ni mjane na mume wake aliaga dunia wakati wa shambulizi la kigaidi lililotokea katika Hoteli ya Dusit D2. 

"Mwanamke huyo aliniambia ni mjane na mume wake aliaga dunia wakati wa shambulizi la kigaidi la Dusit D2 ," "Sikuwa najua mume wake alikuwa hai na pia afisa wa KDF katika kambi ya Nanyuki," alisema jamaa huyo akiomba ulinzi.
Via Tuko News

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527