RAIS MAGUFULI ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA URAIS


Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Rais John Magufuli, leo amechukua fomu za kuwania kuteuliwa na chama chake kushiriki katika kinyang’anyiro cha urais katika uchaguzi mkuu ujao.

Rais Magufuli amekabidhiwa fomu hiyo na Katibu Mkuu wa CCM Dkt Bashiru Ally kwenye Makao Makuu ya chama hicho mkoani Dodoma.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa fomu hiyo, Rais Magufuli amesema anaanza mapema mchakato wa kutafuta wadhamini  ili awahi kurejesha fomu hiyo mapema.

Mwenyekiti huyo wa CCM amesema amekuwa akipigiwa simu na makada wa chama hicho, ambao wamemuahidi kumdhamini.

“Naomba nianze zoezi hili la kutafuta wadhamini, nitaenda mikoa yote kwa sababu nimekuwa nikipigiwa simu wakisema wanataka kunidhamini hivyo nitarejesha fomu yangu kwa wakati,” amesema Rais Magufuli.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527