BALOZI ALI KARUME AJITOSA KUGOMBEA URAIS ZANZIBAR | MALUNDE 1 BLOG

Monday, June 15, 2020

BALOZI ALI KARUME AJITOSA KUGOMBEA URAIS ZANZIBAR

  Malunde       Monday, June 15, 2020

Balozi Ali Karume amechukua fomu kuwania kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa mgombea wa Urais wa Zanzibar katika uchaguzi mkuu ujao.


Akizungumza na waandishi wa habari mjini Unguja, Balozi Karume amesema kuwa endapo atateuliwa kuingia kwenye kinyang’anyiro cha Urais na baadaye kushinda kiti cha Urais wa Zanzibar ataendeleza mazuri yote yaliyofanywa na watangulizi wake.

Pia ameahidi kuimarisha muungano kwa manufaa ya Wanzania wa pande zote mbili za Muungano huo.


“Iwapo nitateuliwa, nategemea kuendeleza dhamira ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kulinda muungano wetu na kuendeleza Sera ya CCM, Dk. Ally Shein, rais wangu amefanya kazi ya kupigiwa mfano hasa kuendeleza sera zilizoanzishwa na Abeid Karume, nia yangu ni kuendeleza yote mazuri,” amesema Karume.


Karume ambaye kwa sasa ni Waziri wa Vijana Utamaduni, Michezo visiwani Zanzibar, amesema endapo atapata nafasi ya kuwa rais wa nchi hiyo, ataboresha utolewaji wa huduma za kijamii, ikiwemo afya, elimu makazi ya watu, ugawaji wa ardhi kwa wananchi wote.

“Nitahakikisha afya inaendelea kupatikana bila malipo,  elimu ipatikane bila malipo, ugawaji ardhi uendelee kwa wananchi wanaohitaji kwa masuala ya kilimo na ujenzi.  Nitajenga makazi bora, Mzee Shein amejenga nyumba nzuri lakini nimeona zinahitaji ukarabati, hilo naahidi tutalifanya pamoja na mengineyo,” amesema Karume


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post