AJALI YA LORI,TREKTA, HIACE YAUA WATU 8,KUJERUHI WATANO IHAYABUYAGA MWANZA


   Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Mwanza Jumanne Muliro

Na mwandishi wetu,Shinyanga Press Club Blog

 Watu nane wamepoteza maisha katika ajali ya gari na wengine watano  kujeruhiwa baada ya Lori mali ya Texas Hardware kugonga Tela la trekta kwa nyuma na kukosa mwelekeo kisha kuligonga gari la abiria 'Hiace' na kusababisha vifo.


Ajali hiyo ilitokea jana Juni 10 majira ya saa 9:45 usiku katika barabara ya Mwanza -Musoma eneo la Ihayabuyaga Kata ya Bukandwe wilayani Magu mkoani Mwanza ambapo tayari wanamshikilia dereva wa lori Boniphace Cliphord Tuju(37) mkazi wa mwanza-Nera


Taarifa iliyotolewa leo Juni 11 na kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Mwanza Jumanne Muliro imesema kuwa, dereva huyo alikuwa anaendesha gari lenye namba za usajili T.322 DCB na Trailer T.1351 DCA na lilikuwa likitoka wilaya ya Busega kwenda Mwanza.


Kamanda Muliro amesema Lori hilo liligonga  tela ya trakta kwa nyuma ambayo ilikuwa haina taa za nyuma yenye namba za usajili T.952 DGW, baada ya kuligonga ilihama njia na kugongana na gari iliyokuwa na abiria kutoka mwanza kwenda magu yenye namba za usajili T.775 DEG.


Alisema gari ya abiria aina ya Nissan inayomilikiwa na  george philipo@msangi ambaye alikuwa dereva wa gari hiyo ambaye alifariki kwenye ajali na abiria wake waliopoteza maisha wote wakiwa ni wanaume na watano kujeruhiwa.


Waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo na miili yao kutambuliwa ni George Msangi dereva wa Hiace mkazi wa Magu,Hamis Masige(35) mwalimu wa Luhenge secondary mkazi wa Lugeye na waliofariki wengine 6 bado hawajatambulika wote ni wanaume.

Majeruhi wa ajali hiyo ambao wanapatiwa matibabu hospitali ya Bugando kuwa ni Ayubu Mindule Mratibu elimu Kata ya Chabula mkazi wa nyanguge,Elias Lutandula(46)mkulima mkazi wa Nyanguge.

Wengine ni Kasabuku Kishela(32)msukuma mkazi wa Magu, Edibini Makubo (20) mwanafunzi wa kidato cha sita Bariadi high school mkazi wa Nyanguge na Elias Francis(44)mkazi wa nyangugambaye amelazwa hospitali ya Magu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527