WAGONJWA WA CORONA UGANDA WAFIKA 281 BAADA YA WENGINE 28 KUONGEZEKA


Wizara ya Afya nchini humo imetangaza ongezeko la Wagonjwa wengine 28 na kufanya jumla ya visa vya Corona nchini humo kufikia 281.

Wagonjwa 21 ni madereva wa malori walioingia Uganda kupitia mpaka wa Elegu wakitokea Sudan Kusini huku 7 ni waliokuwa Karantini baada ya kukutana na madereva waliotangazwa awali.

Kati ya madereva 21, 7 ni raia wa kigeni kutoka Tanzania (4), Congo (1), Burundi (1) na Eritrea (1). Wote wamekabidhiwa kwa nchi zao.

Aidha, Wizara hiyo pia imetangaza jumla ya Wagonjwa waliopona kuwa 69. Jumla ya sampuli zilizopimwa jana na kuleta matokeo hayo ni 2,004.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527