TRUMP ATISHIA KUFUNGA MITANDAO YA KIJAMII NCHINI MAREKANI


Rais wa Marekani Donald Trump anatarajia leo Alhamisi kutia saini kwenye agizo linalolenga mitandao ya kijamii, maafisa wa Ikulu ya White House wamesema, saa chahe baada ya rais huyo kutishia  kufunga makampuni ya mitandao yote ya kijamii, akiyatuhumu kujaribu kuzuia uhuru wa kujieleza.

Wawakilishi hao hawakutoa maelezo zaidi kuhusu yaliyomo kwenye agizo hilo la rais Trump. Haijulikani kwa wakati huu jinsi Donald Trump atakavyopitisha  tishio lake la kufunga kampuni binafsi, ikiwa ni pamoja na Mtandao wa Twitter.

Mzozo huo uliibuka Jumanne wakati Mtandao wa Twitter ulihakiki ukweli wa baadhi ya ujumbe wa Rais wa Marekani Donald Trump alioundika katika ukurasa wake. Ni mara ya kwanza mtandao huo ambao Trump anapendelea zaidi kuutumia unafanya hivyo.

Rais wa Marekani alighadhibishwa na jambo hilo na kushumu mtandao huo kwa kile alichokiita ‘kuingilia kati' uchaguzi wa urais wa mwezi Novemba pamoja na uhuru wa kujieleza.

Twitter ilichukua hatua hiyo ambayo haraka ilichochea mvutano kati yake na Trump, baada ya rais huyo wa Marekani kuandika Tweet mbili akidai kwamba mtindo wa kupiga kura kwa njia ya posta huwa una udanganyifu mwingi.

Ilichofanya Twitter ni kuweka kiungo kingine chini ya ujumbe wa Trump kinachosema "Pata taarifa za ukweli juu ya kura ya njia ya posta,” na baadae kiungo hicho kinampeleka mtumiaji kwenye makala ya habari inayompa taarifa za ukweli kuhusu suala hilo, na orodha ya maelezo yanayopinga madai ya Trump.

Trump mwenye wafuasi wapatao milioni 80 katika ukurasa wake wa Twitter, anasema anautumia mtandao huo wa kijamii kupinga kile anachodai kuwa ni taarifa za upendeleo zinazotolewa na vyombo vya habari.

Trump amekuwa akidai kwamba mtindo wa kupiga kura kwa njia ya posta, una viwango vya juu vya udanganyifu katika wakati ambapo majimbo mengi yanazingatia kuitumia njia hiyo ili kulinda afya ya raia dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19 wakati taifa hilo likiwa linaelekea katika uchaguzi wa rais wa mwezi Novemba.

Credit:RFI


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post