WAGONJWA WA CORONA UGANDA WAFIKA 126


Wizara ya Afya nchini Uganda imesema Madereva wanne wa malori wamethibitishwa kuwa na  Virusi vya Corona na kufanya idadi ya visa nchini humo kufikia 126.


Wawili kati ya Wagonjwa wapya ni Waganda huku wengine wakiwa ni raia wa Kenya na Tanzania. Waganda na Mkenya wanaaminika kuingia Uganda kupitia mpaka wa Elegu na Mtanzania alipimwa katika mpaka wa Mutukula

Wamegundulika baada ya sampuli 1,478 za madereva wa malori kupimwa na Taasisi ya Utafiti wa Virusi Uganda. Hadi sasa sampuli zaidi ya 10,000 za madereva wa malori zimepimwa


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post