WAGONJWA WA CORONA NCHINI UGANDA WAFIKA 203


Wizara ya Afya Uganda imesema kuna ongezeko la wagonjwa wapya 43 wa corona wote wakiwa ni madereva wa malori na kufanya jumla ya maambukizi kufikia 203 kutoka 160.


Miongoni mwa 43 hao 17 ni waganda,14 wakenya,Watanzania 5,raia wa Eriteria 4,raia wa Burundi 2 huku utambulisho wa 1 ukiwa bado haujajulikana.

Sampuli 720 zilizokusanywa kwenye jamii nchini humo hazijaonyesha maambukizi yoyote.

Jumla ya sampuli zilizofanyiwa uchunguzi ni 2558,waliopona wakiwa 63.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527