UTEUZI WA WAKURUGENZI WA MAMLAKA ZA MAJISAFI NA USAFI WA MAZINGIRA – ARUSHA NA SUMBAWANGA


 Waziri wa Maji Mhe. Prof. Makame Mbarawa (Mb) amefanya uteuzi wa Wakurugenzi Watendaji wa Mamlaka za Maji na Usafi wa Mazingira za Arusha na Sumbawanga kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia  tarehe 15 Mei, 2020.

Taarifa ya Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Prof. Kitila Mkumbo imewataja walioteuliwa kuwa ni Mhandisi Justine Gordian Rujomba anayekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha (AUWSA), na Mhandisi Gibon Nzowa anayekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Sumbawanga (SUWASA).

Uteuzi huo umefanyika chini ya Sheria Namba 5 ya Usambazaji Maji Usafi wa Mazingira ya mwaka 2019. Aidha,  Wakurugenzi walioteuliwa watakuwa Makatibu wa Bodi za Wakurugenzi katika mamlaka hizo.

Kitengo cha Mawasiliano


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527