WABUNGE WENGINE WAWILI CHADEMA WATANGAZA KUHAMIA NCCR- MAGEUZI


Wabunge wa Viti maalumu kupitia CHADEMA   Joyce Sokombi na Sussane Masele  wametangaza kuhama chama hicho na kujiunga na Chama cha NCCR-Mageuzi mara baada ya kuhitimishwa kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Wabunge hao wameeleza sababu za kuhama kuwa  ni pamoja  na CHADEMA kutokuheshimu katiba yake ikiwa ni pamoja  na wabunge wanne wa chama hicho kufukuzwa uanachama bila kupewa nafasi ya kusikilizwa. 

"Wabunge wa viti maalum kila mwezi tunachangia chama Milioni 1.5, kila mmoja amechanga milioni 62, tuko wabunge 37 hivyo tumechangia jumla ya Bilioni 2.2. hatulalamiki kuchanga kwani ipo Kikatiba. Matumizi ya fedha hizi hayajawahi kuwekwa wazi na haturuhusiwi kuhoji popote

"Madaraka ndani ya CHADEMA yanahodhiwa na wachache wengi wao wakiwa wanaume na hivyo kuwepo mwanya wa unyanyasaji wa kijinsia na kingono" Wamesema Wabunge hao.


Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527