Picha : CHAMA CHA MADAKTARI TANZANIA,SHIRIKA LA UTAFITI HPON WATOA MSAADA WA VIFAA KINGA KUKABILIANA NA CORONA SHINYANGA


Chama Cha Madaktari Tanzania (Medical Association of Tanzania – MAT) na Shirika la Utafiti HPON (Heath For A Prosperous Nation) wametoa msaada wa Vifaa Kinga vyenye thamani ya shilingi Milioni 4.5 kwa ajili ya kukabiliana na Maambukizi ya Virusi vya Corona (COVID -19) katika mkoa wa Shinyanga.

Vifaa kinga hivyo ambavyo vitatumika katika vituo vya kutolea huduma za afya mkoani Shinyanga vimekabidhiwa na wadau hao wa sekta ya afya leo Ijumaa Mei 22,2020 kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile.

Vifaa vilivyotolewa na Shirika la Utafiti HPON (Heath For A Prosperous Nation) ni pamoja na Barakoa ‘Face Masks’ 2500, Ngao za uso ‘Face Shields’ 50 na Nguo maalumu za kuvaa wakati wa kuhudumia wagonjwa (PPE) 10 vyote vikiwa na thamani ya shilingi 3,875,000/=.

Aidha Chama Cha Madaktari Tanzania (MAT), kimetoa msaada wa Barakoa ‘Surgical Masks’ 250,Clean Gloves 250, Vitakasa mikono ‘Hand Sanitizer’ 9 na sabuni za kunawia ‘Hand soap’ 10 vyenye thamani ya shilingi 640,000/=.

Wakizungumza wakati wa kukabidhi vifaa kinga hivyo, Mwakilishi wa Chama Cha Madaktari Tanzania (MAT) Kanda ya Ziwa, Dkt. Tryphone Rwegasira na Dkt. Emmanuel Katabaro kutoka Shirika la Utafiti HPON wamesema vifaa hivyo vitasaidia katika mapambano dhidi ya COVID – 19 mkoani Shinyanga.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile amewashukuru wadau hao wa afya kwa mchango huo mkubwa katika kukabiliana na Ugonjwa Corona huku akibainisha kuwa vifaa hivyo vitatumika kwenye vituo vya kutolea huduma za afya mkoani Shinyanga.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Sehemu ya Vifaa Kinga vilivyotolewa na Chama Cha Madaktari Tanzania (Medical Association of Tanzania – MAT) na Shirika la Utafiti HPON (Heath For A Prosperous Nation) vyenye thamani ya shilingi Milioni 4.5 kwa ajili ya kukabiliana na Maambukizi ya Virusi vya Corona (COVID -19) katika mkoa wa Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kushoto ni Mwakilishi wa Shirika la Utafiti HPON (Heath For A Prosperous Nation) Dkt. Emmanuel Katabaro akimkabidhi Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile nguo maalumu za kuvaa wakati wa kuhudumia wagonjwa (PPE). Katika kukabiliana na Ugonjwa wa Corona mkoani Shinyanga, Shirika la Utafiti HPON  limechangia Barakoa ‘Face Masks’ 2500, Ngao za uso ‘Face Shields’ 50 na nguo maalumu za kuvaa wakati wa kuhudumia wagonjwa (PPE) 10 vyote vikiwa na thamani ya shilingi 3,875,000/= .
Wa pili kushoto ni Mwakilishi wa Shirika la Utafiti HPON (Heath For A Prosperous Nation) Dkt. Emmanuel Katabaro akimkabidhi Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile vifaa kinga kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa wa Corona. Wa kwanza kushoto ni Katibu wa Afya mkoa wa Shinyanga, William Mambo. Wa kwanza kulia ni Mwakilishi wa Chama Cha Madaktari Tanzania (MAT), Dkt. Tryphone Rwegasira.
Mwakilishi wa Chama Cha Madaktari Tanzania (MAT) Kanda ya Ziwa, Dkt. Tryphone Rwegasira akimkabidhi Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile (katikati) vitakasa mikono,gloves na Barakoa. Katika kukabiliana na Ugonjwa wa Corona mkoani Shinyanga, Chama Cha Madaktari Tanzania (MAT) , limetoa msaada wa  Barakoa ‘Surgical Masks’ 250,Clean Gloves 250, Vitakasa mikono ‘Hand Sanitizer’ 9 na sabuni za kunawia ‘Hand soap’ 10 vyenye thamani ya shilingi 640,000/=. Kushoto ni Katibu wa Afya mkoa wa Shinyanga, William Mambo.
Mwakilishi wa Chama Cha Madaktari Tanzania (MAT) Kanda ya Ziwa, Dkt. Tryphone Rwegasira akimkabidhi Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile (katikati) vitakasa mikono,gloves na Barakoa.
Baada ya makabidhiano ya vifaa kinga kukabiliana na COVID -19 :Mwakilishi wa Chama Cha Madaktari Tanzania (MAT) Kanda ya Ziwa, Dkt. Tryphone Rwegasira (kulia) na Dkt. Emmanuel Katabaro kutoka Shirika la Utafiti HPON (wa pili kushoto) wakipiga picha ya kumbukumbu na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile (wa pili kulia) na Katibu wa Afya mkoa wa Shinyanga, William Mambo (wa kwanza kushoto).
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527